NBC YAWAZADIA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA UPEWE
Meneja
Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto), akizungumza kwa
simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo
jijini Dar es Salaam jana. Wengine kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha
Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Mkuu wa Idara ya
Huduma za Rejareja za Kibenki , Mussa Jallow, Meneja katika Kitengo cha
Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania (GBT), Abdallah Hemedi. Wateja wanne walishinda
pikipiki na wawili jenereta.
Mkuu
wa Idara ya Huduma za Rejareja za Kibenki wa Benki ya Taifa ya Biashara
( NBC) , Mussa Jallow (katikati) akizungumza wakati wa droo ya kwanza
ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Wengine kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo,
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew
Massawe, Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye
na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Abdallah
Hemedi. Wateja wanne walijishindia pikipiki na wawili jenereta.



No comments:
Post a Comment