Ziara ya Rais Geita: Afisa Usalama bandia anaswa akimsogelea Kikwete
GEITA: Katika
hali ambayo inazidisha mashaka juu ya Usalama wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Mtu mmoja ambaye hajatambulika nia
yake, amefanikiwa kujipenyeza katika msafara wa Rais na kujifanya
miongoni mwa walinzi wa msafara.
Mtu
huyo ambaye baada ya kunaswa amekutwa na vitambulisho bandia,
alifanikiwa kujipenyeza katika mkutano wa kwanza wa ziara ya Rais
wilayani Bukombe mkoani Geita, ambapo kulikuwa na sherehe za uzinduzi wa
barabara ya Lami ya Bwanga hadi Uyovu Lunzewe yenye urefu wa km 45
ambayo ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete siku hiyo Novemba
9 mwaka huu.
Akiwa
kama afisa usalama alikuwa akizuia baadhi ya watu kufika maeneo maalum
yaliyoandaliwa mahususi kwa ulinzi, lakini pia alikuwa akipitapita
kukagua baadhi wa watu wakiwamo na waandishi wa habari huku akiwapanga
namna ya kukaa vyema kabla msafara wa Rais kuwasili eneo la tukio.
Katika
mkutano huo wa kwanza alifanikiwa kupita salama kwani baada ya mkutano
huo kumalizika, aliweza kupata usafiri na kuondoka na msafara umbali wa
km 53 na kufika Ikulu ndogo ya Bukombe, ambako msafara uliitulia kwa
muda na wageni kupata chakula, kisha kuelekea katika mkutano wa pili wa
hadhara mjini Ushirombo.
Hata
hivyo, huko hakuweza kufanikiwa, Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa
shirikiana na Maofisa Usalama wa Taifa, lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu
huyo kama inavyoonyesha (Pichani Juu) akiwa
ameshikwa chini na Ulinzi wa Askari polisi na afisa usalama akitolewa
katika ya mkutano wa Rais Kikwete uliofanyika katika Uwanja wa Kituo cha
mabasi Ushirombo.
Mtu
huyo ametambulika kwa jina la Kwamani Juma anakadiriwa kuwa na umri kati
ya 43-46, alikamatwa Novemba 9 mwaka huu, eneo la Ushirombo katika
mkutano wa hadhara akiwa amejipanga kama maaofisa Usalama karibu na
jukwaa kuu alilokuwa amekaa Rais Jakaya Kilwete.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amethibitisha kukamatwa kwa afisa
huyo bandia, alisema "Ndiyo… amekamatwa, si umeona kwenye mkutano
kilichotokea, sasa unataka nieleze nini zaidi," alielza Kamanda Paul.source hapa
No comments:
Post a Comment