Header Ads

MRADI WA INTERNATIONAL INSPIRATION WANDAA MAFUNZO YA MAAFISA MICHEZO ZANZIBAR.

 Mkuu wa Chuo cha Michezo Tanzania Allen Alex, akisisitiza kitu, alipokua akizungumza na Maafisa Michezo wa Wilaya na Walimu wa Skuli mbalimbali za Zanzibar hawapo pichani, kushoto kwake Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis, Katibu mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) Hasan Khairallah katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Michezo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Maafisa Michezo wa Wilaya na Walimu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis hayupo pichani, kabla ya kuyafungua mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis, akizungumza na  Maafisa Michezo wa Wilaya na Walimu mbalimbali, mafunzo hoyo yataanza kesho kwa muda wa siku 3 katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Michezo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar).

No comments:

Powered by Blogger.