Taarifa zilizolifikia Mwananchi Jumapili na kuthibitishwa na Zitto jana
jioni zilieleza kuwa Eurodad ambao ni mtandao wa mashirika yasiyo ya
kiserikali 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, yanayojihusisha na masuala ya
kufuatilia madeni ya nchi zinazoendelea, kwa muda sasa umekuwa
ukipambana na watu wanaokwepa kulipa kodi. Picha na Maktaba.
DAR ES SALAAM.
WAKATI ikisubiriwa ripoti ya uchunguzi wa Tume
Maalumu iliyoundwa kwa Azimio la Bunge kuchun
guza kashfa ya vigogo
walioficha Sh323.4 bilioni katika benki nchini Uswisi, Shirika la
Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo (Eurodad), leo
linaanza kuwachunguza walioficha mabilioni hayo ya fedha nchini humo.
Kazi hiyo ya uchunguzi inaanza leo hadi Novemba 5,
mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine watafanya ziara ya uchunguzi
kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya.
Uchunguzi huo utafanywa na jopo la wataalamu
waliobobea katika masuala ya kodi na maendeleo na wataongozwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ambaye pia
ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa bungeni kwa hoja
binafsi ya Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwishoni
mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Kufuatia hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne
Makinda liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia
Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo
bungeni.
Ripoti ya Tume hiyo iliyoundwa na Serikali kwa
Azimio la Bunge ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana, ikiongozwa na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, mpaka sasa
tayari imewahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na
wafanyabiashara.
Muda wa tume hiyo kufanya uchunguzi unakamilika
mwezi huu na inatarajiwa katika mkutano ujao wa Bunge unaoanza Oktoba 29
mjini Dodoma, itawasilisha ripoti hiyo.
Taarifa zilizolifikia Mwananchi Jumapili na
kuthibitishwa na Zitto jana jioni zilieleza kuwa Eurodad ambao ni
mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali 48 kutoka nchi 19 za Ulaya,
yanayojihusisha na masuala ya kufuatilia madeni ya nchi zinazoendelea,
kwa muda sasa umekuwa ukipambana na watu wanaokwepa kulipa kodi.
“Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga
utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya
kimataifa kwa nchi zinazoendelea,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kesho Zitto atakutana
na Waziri wa Fedha wa Uswisi na maofisa wa benki mbalimbali na asasi za
kiserikali zilizopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Geneva.
“Zitto pia atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi
ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za
kimataifa ili kuzuia unyonywaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na
kampuni kubwa za kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment