RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAMA SALMA WATEMBELEA WILAYA ZA WANGING'OMBE NA MAKETE,MKOANI NJOMBE
Rais
Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha
VETA cha Wilaya ya Makete tarehe 19.10.2013 kilichojengwa katika Mji wa
Iwawa, Makao Makuu ya wilaya hiyo. KatIka hafla hiyo uongozi wa Chuo
hicho umeamua kukipa jina la Jakaya Kikwete kwa jitihada zake
alizowezesha wilaya ya Makete kuwa ya kwanza nchini kuwa na chuo cha
VETA cha wilaya. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Elimu NA Ufundi Dr.
Shukuru Kawambwa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine
Matiro.
Rais
Jakaya Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma wakitembelea Chuo cha VETA
cha Makete na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo
wa chuo hicho mara tu baada ya kukizindua rasmi tarehe 19.10.2013.
Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma wakipata maelezo ya namna gani ya kupata
udongo unaofaa kwa ajili ya kufyatua matofali kutoka kwa Geofrrey Sanga
na Abel Mbilinyi, wanachuo wa mwaka wa kwanza wa chuo hicho.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali waliofika
kuwapokea wakati walipowasili kwenye kijiji cha Kipengere tarehe
19.10.2013.
No comments:
Post a Comment