Taarifa
zilizotufikia katika dawati letu la habari la BAMIZA BLOG kutoka kwenye
vyanzo mbalimbali vya Habari Mjini Morogoro zinatutaarifu kuwa
aliyekuwa Mtangazaji mahiri na nguli katika tasnia ya habari na
utangazaji Julius Nyaisanga, aliyekuwa mfanyakazi wa Abood Media mjini
Morogoro amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi.
Marehemu Nyaisanga alikuwa akisumbuliwa na Shinikizo la damu na sukari .
Wakati
wa uhai wake Marehemu Nyaisanga aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya
IPP media ambapop aliwahi kuwa mkurugenzi wa Radio One pamoja na radio
Tanzania wakati huo ikiitwa RTD
Marehemu ameacha mjane na watoto watatu
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema Peponi Amin
No comments:
Post a Comment