MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA ELIMU BEIJING
Profesa Shirley Walters, Mkurugenzi wa
Idara ya Elimu ya masafa marefu katika Chuo Kikuu cha Western Cape
Afrika kusini akimkabidhi Meya Jerry Silaa notebook ya maadhimisho ya
miaka kumi ya mihadhara ya Mwalimu Nyerere inayofanyika kila mwaka
chuoni hapo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Jerry
Silaa akizungumzia kampeni yake ya Mayor’s Ball ‘Dawati ni Elimu katika
mkutano wa kimataifa wa Beijing International Conference on Learning
Cities ambapo alikuwa mmoja wa watoa mada.
Kutoka kushoto Mwezeshaji Mr Ahlin
Jean-Marie, Meya Jerry Silaa, DRC Congo Waziri wa Elimu Mh, Therese
Olenga Kalond, Meya Comlan Lome, Togo na Kamishina wa Elimu Farouk Iya
Sambo Kano State Nigeria. Jukwaani Meya Haskins Nkaigwa Gaborone,
Bostwana.
.apata nafasi ya kunadi kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’
Mstakihi Meya wa Manispaa ya Ilala, Ndugu
Jerry Silaa hivi karibuni alipata fursa ya kuhudhuria mkutano wa
Beijing International Conference on Learning Cities ambapo alipata
nafasi ya kuzungumzia kampeni yake ya Mayor’s Ball ‘Dawati ni Elimu’
kama mmoja wa watoa wa mada kwenye mkutano huo ulioratibiwa na shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO).
No comments:
Post a Comment