JK AFUNGA SEMINA MAALUM KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA CCM, NCHINI MJINI DODOMA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mweneyekiti wa CCM,
Rais Jakaya Kikwete alipowasili Makao Makuu ya CCM, Jengo la White
House, mjini Dodoma, kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM
ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM (Bara) Philip Mangula.
Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha,
alipowasili ukumbini kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM
ngazi za wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, 2013 mjini Dodoma. Mafunzo
hayo yaliyokuwa ya siku nne yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM,
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana.
Ukumbi ukilipuka kwa mbinje, nderemo na vifijo, Mwenyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete alipowasili ukumbini, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma
kufunga mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula,
baada ya kuwasilini ukumbini na kulakiwa kwa shangwe na wahitimu wa
mafunzo kwa wa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya
nchini mjini Dodoma, jana, Oktoba 24, 2013.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kufunga
mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa hapa
nchini, mjini Dodoma , jana , Oktoba 25, 2013. Kushoto ni Kinana na
Kulia ni Mangula.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza namna
mafunzo hayo yalivyoandaliwa na Idara yake ya Itikadi na Uenezi na
kumalizika kwa mafanikio makubwa.
Baadhi ya viongozi wa Jumuia na Sekretarieti wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akitazama bango jipya la
picha za wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, baada ya mabango hayo kugawiwa
kwa washiriki wa mafunzo hayo ukumbini, wakati wa kufungwa mafunzo hayo.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihamasisha baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kifunga mafunzo hayo.
VYETI TUTAGAWA KAMA HIVI: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
akisema hivyo huku akimshika mkono mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,
Bashir Nkoromo, kabla ya kuanza kugawa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo kwa
watendaji na viongozi wa CCM, ngazi za wilaya na mikoa, jana Oktoba 24,
2013, mjini Dodoma. Nkoromo ambaye ni Mpigapicha Mwandamizi wa Uhuru
Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru,Mzalendo na
Burudani, ni Katibu Msaidizi katika Kitengo cha Mawasiliano na Umma,
Idara ya Itikadi na Uenezi, CCM, Taifa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa
Makatibu wa CCM wa mikoa, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven
Kazidi, alipofunga mafunzo ya utendaji bora kwa watendaji na viongozi wa
CCM ngazi za wilaya na mikoa., jana, Oktoba, 24, Makao Makuu ya CCM
mjini Dopdoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula
na Watatu ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdultahman Kinana. Zaidi ya makatibu
wa CCM wa mkoa wa wilaya zote nchini wamehitimu mafunzo hayo. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment