MJENGWABLOG INAWAKARIBISHA WAHARIRI MKOANI KWETU IRINGA...!
Ndugu zangu,
Kwa niaba ya Wana-Iringa na hususan wadau wa habari wa mkoani Iringa, Mtandao wa KwanzaJamii.com na
Mjengwablog. com unachukua fursa hii kuwakaribisha mkoani kwetu Iringa,
wahariri wanachama wa Jukwaa la Wahariri hapa nchini.
Ni heshima kubwa kwetu Wana-Iringa kwa Jukwaa la Wahariri kuichagua Iringa kama mahali pa kufanyia Mkutano wao Mkuu wa Mwaka.
Ni
faraja pia, tukikumbuka tukio la kuawa kwa ndugu yetu na mwanahabari
mwenzetu Daud Mwangosi mwaka mmoja uliopita. Tukikumbuka pia tukio la
miezi ya karibuni la kujeruhiwa vibaya kwa mwanahabari na mhariri wa
miaka mingi hapa nchini, Absalom Kibanda.
Ni
jambo la kutia matumaini pia, kuwa moja ya ajenda za Mkutano huo wa
Wahariri unaoanza leo Ijumaa na kumalizika kesho Jumamosi ni kujadili
masuala ya Usalama wa Wanahabari.
Ni
matumaini yetu, kuwa Wahariri kupitia Mkutano wao huu wa Iringa , na
wakiwa Iringa yenye hali ya hewa nzuri, Iringa yenye amani, utulivu na
isiyo na hata foleni za barabarani..
Naam,
wakiwa mbali sana na news rooms zao, Wahariri hao watapata fursa ya
kujadiliana kwa kina na hatimaye kutoka na ' Azimio La Iringa' lenye
maslahi kwa tasnia ya habari nchini na jamii kwa ujumla.
Na
huko mitaani Iringa wahariri muwachangie Wana-Iringa kwa kununua bidhaa
zinazotengenezwa Iringa. Msisahau pia kula vyakula vyetu vya Iringa
ikiwamo na vinywaji pia.
Si
mnajua, Iringa tuna maji ya chemchem kama vile Maji Afrika, ya Mufindi,
Image na yale yanayotirika kutoka kwenye miti...! Tuna pia bidhaa bora
zitokanazo na maziwa ya ng'ombe wafugwao hapa Iringa. Hii ni pamoja na
jibini na maziwa bora na maarufu nchini yenye chapa ya 'Asas Milk'.
Na
kwenye mechi yenu ya kesho dhidi ya wanahabari wa Iringa matokeo
hayahitaji utabiri wa Sheikh Yahya. Kwa vile kuna ng'ombe anashindaniwa,
basi, ndugu zangu Wahariri mtambue, kuwa, kwa Mnyalukolo, kwenye
kugombania nyama, hakubali matokeo mengine isipokuwa ushindi tu..!
KwanzaJamii.com na Mjengwablog inawatakia ukazi mwema mkiwa Iringa.
No comments:
Post a Comment