MEYA SILAA AJA NA KAMPENI KABAMBE YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA SANAA
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa (wa pili kushoto) akizungumza
na waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’
kupitia wasanii mbalimbali wa kuchora nchini. Kulia kwake ni Msanii
Robin Mtila na Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro,
Trevor Saldanha na Mustafa Hassanali Mratibu wa Kampeni hiyo.
Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha akizungumzia
mchango wa hoteli yake katika kampeni ya Dawati ni Elimu yenye kauli
mbiu ya "Kalisha mmoja boresha Elimu".
Mchoraji Robin Mtila akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake ambapo
ameelezea umuhimu wa sekta ya Elimu katika fani ya sanaa nchini.
Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd Dhmy Jog akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kampuni yake kuchangia Tsh 10 milioni kwenye kampeni
hiyo ya kuondoa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari
nchini.
Baadhi wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha kubwa la Sanaa lenye lengo la kuchangia kampeni ya Dawati ni Elimu.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na
wasanii wa Sanaa ya Uchoraji pamoja na baadhi ya wadhamini wa kampeni
hiyo. .Kampeni ya Dawati ni Elimu yakusanya Tsh 1bilioni mpaka sasa lengo ni kufikia Tsh 4.98bilioni .atoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha la mwaka dawati ni elimu
No comments:
Post a Comment