Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali wa Bunge la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe
---
Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni
na Maendeleo, European Network on Debt
and Development (Eurodad) watafanya ziara ya kiuchunguzi kuhusu
masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya kuanzia tarehe 20 Oktoba
mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013. Uchunguzi huo utaendeshwa na wataalamu
waliobobea wa masuala ya kodi na maendeleo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali wa Bunge la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la
uchunguzi huo.
Eurodad ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala
ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki.
Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia
ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea.
Zitto amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya kutaka Watanzania
waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa mashtaka.
Mwaka 2012
aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa Azimio la Bunge ya kutaka
uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na kufichwa nje kama Uswiss. Kikosi Kazi
cha Serikali kutekeleza Azimio hilo la Bunge kinatarajia kuwasilisha taarifa
yake katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge. Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba
Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi
zisizo za kiserikali zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa
Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za
kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na Makampuni
makubwa ya Kimataifa.
Baada ya Geneva Zitto atatembelea nchi za
Luxembourg na Brussels kabla ya kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa
Jopo la Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu
yenye mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.
Zitto atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu
masuala ya kodi za kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government
Partnership). Mwenyekiti wa PAC Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa
PAC Uingereza Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa
mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa makampuni ya kimataifa kulipa kodi
zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax Havens’ kukwepa kodi na
kufukarisha nchi za Kiafrika.
Zitto invited to annual
OGP Summit
The Kigoma North Member of Parliament and Chairman
of the Public Accounts Committee (PAC), Hon Zitto Kabwe has been invited for
the annual Open Government Partnership (OGP) Forum which kicks off in London at
the end of the month.
The OGP Summit is a chance to promote tax and
illicit issues to new audiences, to encourage new commitments in country action
plans.
Hon Zitto, who also serves as Deputy Leader of
Official Opposition in the Parliament, will serve in the panel which will
discuss tax and illicit flows, which is among themes to be deliberated during
the summit.
The OGP is a global platform for domestic reformers
committed to making their governments more open, accountable, and responsive to
citizens. Tanzania is among countries which have signed its membership to the
OGP.
Hon Zitto has great interest on tax avoidance
through illicit transfers and last year he tabled private motions which lead to
the adoption of a Parliament Resolution compelling the government to
investigate a number of individuals who have illicitly stashed billions of
dollars abroad.
The fact finding mission will see its members
interact with UN Tax Committee, OECD, EU as well as key European governments.
They will visit a number of European cities namely Geneva, Paris, Luxembourg,
Brussels and Oslo.
Ends
Issued
by;
Parliamentary
Office of Hon. Zitto Kabwe MP
Dar es
Salaam
October
19, 2013
No comments:
Post a Comment