DAR ES SALAAM.
KESI ya Kikatiba inayomkabili Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), inaanza kuunguruma
leo katika Mahakama Kuu ya Tanz
ania Kanda ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo ilifunguliwa kwa ushirikiano wa Kituo
cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na
TLS, wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kwa kauli aliyoitoa Bungeni
kuhusu polisi kuwapiga raia wanaokaidi amri.
Walalamikaji hao wanadai kuwa kauli hiyo ni amri kwa vyombo vya dola kutekeleza sheria ya kuwapiga wananchi, wakati wa vurugu.
Hata hivyo Pinda na AG katika majibu yao,
wamewasilisha pingamizi la awaliambalo pamoja na mambo mengine wanadai
kuwa walalamikaji na watu waliorodheshwa katika kesi hiyo, hawana
mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
Pingamizi hilo limepangwa kusikilizwa leo na jopo la majaji linaloongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment