Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akikagua ujenzi wa nyumba 851
kwa ajili ya kuuzia wafanyakazi wa serikali baada a kuweka jiwe la
msingi jana katika eneo la Mabwe Pande Jijini la Dar es Salaam. . Kulia
ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli. Picha na Salim Shao.
DAR ES SALAAM. WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa watumishi wa Serikali ambao wanadaiwa mikopo ya nyumba kulipa madeni yao mara moja na kuonya kwamba ikiwa watashindwa kulipa, watany ang’anywa nyumba hizo na watakopeshwa watu wengine.

Dk Magufuli ameibuka na hoja hiyo mpya, zikiwa ni
siku chache tangu alipopigwa ‘stop’ na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kutekeleza sheria ya kuondoa msamaha wa asilimia tano kwa mizigo
inayozidi kwenye malori, hali ambayo ilizusha mvutano mkubwa baina ya
Serikali na wasafirishaji wa mizigo nchini.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi
kuzindua ujenzi wa nyumba 851 za watumishi wa Serikali eneo la
Mabwepande jijini Dar es Salaam, Dk Magufuli alisema watumishi 2500
hawajalipa mikopo ya nyumba walizonunua.
Dk Magufuli alionya kuwa atafuatilia suala hilo na
kuhakikisha madeni hayo yanalipwa mara moja, huku akimwomba Makamu wa
Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal kumuunga mkono kwenye jambo hilo, ambalo
ni utekelezaji wa sheria za nchi.
“Naomba ifahamike kwamba tunapojenga nyumba kwa
ajili ya kuwakopesha watumishi wa umma tunataka kuboresha makazi yao.
Pia fedha tunazokusanya zinasaidia kujenga nyumba zaidi,” alisema Dk
Magufuli. Hata hivyo alisema hadi sasa watumishi wa Serikali 4,900 ambao
walikopa nyumba hizo tayari wamelipa madeni.
“Mimi nafanya kazi kwa kufuata sheria na kila
mtumishi wa Serikali anafahamu jambo hilo, hivyo watu ambao wanajua
tunawadai wakae kwa tahadhari, kwani ndani ya mwezi mmoja kama
hawatalipa tutawachukulia hatua bila kupuuzia,” alionya Magufuli.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Dk Magufuli kutangaza
kunyang’anya nyumba hizo, kwani alifanya hivyo mwishoni mwa Machi mwaka
jana pale alipouagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
kuwapa siku saba watu wote walionunua nyumba hizo kulipa madeni yao.
Dk Magufuli aliwataka TBA kutoa ilani ya maandishi
inayowataka wahusika walipe fedha hizo ndani ya wiki moja vinginevyo
wangenyang’anywa kwa maelezo kwamba wanachelewesha malengo ya TBA
kujenga nyumba zaidi.
Hata hivyo, hakuna taarifa zozote zilizowahi kutolewa kuhusu kutekelezwa kwa amri hiyo iliyotolewa zaidi ya miezi 18 iliyopita.
Hata hivyo, hakuna taarifa zozote zilizowahi kutolewa kuhusu kutekelezwa kwa amri hiyo iliyotolewa zaidi ya miezi 18 iliyopita.
Jana, Makamu wa Rais, Dk Bilal alimuunga mkono
Magufuli akisema: “Naunga mkono tamko la Waziri wa Ujenzi kwamba ni
lazima watumishi wa Serikali ambao wanakopeshwa nyumba walipe haraka ili
fedha hizo zisaidie kujenga nyumba nyingine.”
Dk Bilal alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 851, kwenye eneo la Bunju ‘B’
Kinondoni, Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga,
alisema ujenzi huo unafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
iligharimu Sh2 bilioni na awamu ya pili Sh1 bilioni.
“Nyumba 851 zinazojengwa Bunju B ni sehemu ya
ujenzi wa nyumba 4,400 katika Mkoa wa Dar es Salaam na nyumba 10,000 kwa
nchi nzima,” alisema Mwakalinga.
Hafla hiyo ilisimama takriban kwa dakika 10 wakati
Dk Bilal akitaka kuhutubia baada ya jenereta kushindwa kufanya kazi,
hivyo kumlazimu kurudi kuketi kwenye kiti hadi umeme uliporejea.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alilazimika kwenda kufuatilia suala hilo na mafundi waliokuwapo walifanikiwa kuunganisha mashine za kipaza sauti na umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), hivyo Makamu wa Rais aliendelea kuhutubia. MWANANCHI

No comments:
Post a Comment