KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AFUNGA KIKAO CHA BAJETI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI LA MAGEREZA MKOANI, MOROGORO
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba ya
ufungaji wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kilichofanyika kwa
muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Kikao hicho cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha
2013/2014 kilifunguliwa rasmi Oktoba 21, 2013 na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb). Baadhi
ya Wajumbe Washiriki wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa
mwaka wa fedha 2013/2014 wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya
ufungaji wa Kikao hicho katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro. Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini( wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yenye miradi ya Shirika la Uzalishaji
la Magereza kwa waliosimama katika picha( wa pili kushoto) ni Kamishna
wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile( wa tatu kulia) ni
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili
kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga( wa kwanza kushoto)
ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ndg. Janabi(wa kwanza kulia) ni Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James
Selestine. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment