DK. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA WATENDAJI WA CCM, DODOMA
Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua
semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
mikoa na wilaya nchini, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu lengo la mafunzo hayo.
Katibu
wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akitoa neno la utangulizi kabla
ya kumkaribisha Kartibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza
kwenye semina hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Dodoma, leo kwa ajili ya kufungua semina hiyo.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili
katika ukumbini kwa ajili ya kufungua semina ya mafunzo kwa watendaji na
viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya, leo kwenye Jengo la White
House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
Wajumbe wakishangilia, Dk. Shein alipowasili ukumbini. Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakishangilia baada ya semina yao kufunguliwa na Dk. Shein.
Makatibu
wa NEC, Zakiah Meghji (Uchumi na Fedha) na Mohammed Seif Khatib
(Oganaizesheni) wakifuatilia kwa makini hali ya mambo ukumbini wakati wa
semina hiyo.
Dk. Shein akiwaaga wajumbe na viongozi wengine baada ya kufungua semina hiyo.
No comments:
Post a Comment