ZAMBIA MABINGWA AFRIKA 2012

Mchezo huo ulimaliza dakika 90
za kawaida, kabla ya kwenda muda wa ziada, na hadi katika mikwaju ya
penati.
Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga
ambapo Kolo Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.
Ivory Coast
wataendelea kusubiri kunyakua kombe hilo, licha ya kuwa na wachezaji
kadhaa wanaocheza Ulaya hasa katika Ligi Kuu ya England.
Tembo wa
Ivory Coast walipoteza katika mchezo wa fainali mwaka 2006 dhidi ya
Misri kwa mikwaju ya penati.
Lakini kwa Chipolopolo, ambao
wamewahi kushika nafasi ya pili mara mbili, wamemaliza kwa ushindi kwa
kuhanikizwa na vifo vya wachezaji wenzao mwaka 1993, baada ya ndege yao
kuanguka karibu na uwanja ilipochezewa fainali mjini Libreville.
Mara
ya mwisho kwa timu hiyo kutoka Kusini mwa Afrika kufika fainali ilikuwa
mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 wa nchi hiyo kupata
ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Gabon.
Wakielekea katika
mchezo wa fainali, wachezaji hao wa sasa walisema wanahisi nguvu
kutokana na kukumbuka janga lililowapata wenzao.
Kwa kushinda
mchezo wa fainali, wameonesha dhamira ya kuwashinda wapinzani wao ambao
walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment