Rais
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya
Longido muda mfupi baada ya kuwasili wilayani hapo ambapo aliongoza
shughuli ya kutoa msaada wa ng’ombe zaidi ya elfu ishirini na tano na
mbuzi zaidi ya elfu kumi na tano kwa wakazi wa wilaya za
Longido,Ngorongoro na Monduli ambao mifugo yao yote iliangamia wakati wa
kiangazi kikali.(photo by Freddy Maro) Mmoja
wa wazee wa Kimasai akimuombea dua Rais Jakaya Kikwete wilayani Longido
Jumapili, wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa mradi wa Serikali wa
uwezeshaji mifugo (seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo
yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 iliyofanyika
wilayani longido jumapili. (PICHA NA FRED MARO) Mwanafunzi
Godlisten Ole Olais anayesoma Kidato cha Pili katika Shule ya
Sekondari ya Longido, akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi
baada ya Rais kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza
uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa
kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa
2008-2009 na 2009-2010 zilizofanyika wilayani longido jumapili.
Viongozi wa kabila la Kimasai (Laigwenani) wakimpa Rais Jakaya Kikwete
zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi
ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
Mzee wa
Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano
na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji
waliopoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za
Longido,Ngorongoro na Monduli Baadhi
ya vijana wakiwa juu ya mti kumuona na kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete
No comments:
Post a Comment