Mdhamini
wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume
akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa
kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na
wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa
Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na
michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa
Yanga. Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini
katika michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo
akamuomba mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo.
Mgeni
rasmi katika hafla ya timu ya Yanga kutimiza miaka 77 Dk Fenella
Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo
akizungumza katika hafla hiyo, huku Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga
akifurahia jambo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck
Sadik na kushoto ni mdhamini wa Yanga Mama Fatma Karume.
Katibu
Mkuu wa Yanga Selestini Mwesigwa akipiga mamombi kabla ya kuanza kwa
hafla hiyo kulia ni George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro na
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam Sadik Meck Sadik.
Wadau
kutoka Peacock Hotel wakijadiliana jambo ili kuhakikisha sherehe hiyo
inafana zaidi.
Ancle
Hashim Lundenga kulia ndani kama unavyomuona akiwa ametulia kitini Kutoka
kulia ni Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic
shabiki mkubwa wa Yanga Emmanuel Mpangala na Kocha msaidizi wa timu hiyo
mwenye (Mzuka Mwingi) Fred
Felix Minziro wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla hiyo.
Kulia
ni wanachama wa Yanga Mh. Mudhihir Mudhihir kulia na Jaji Mkwawa wakiwa
katika hafla hiyo jana uziku.
Mashabiki
ha wa pia walikuwepo kuipa tafu klabu yao.
Kundi
la THT likitumbuiza katika hafla hiyo
Hii ndiyo mandhari ya ukumbi inavyoonekana
katika picha. (KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOG)
No comments:
Post a Comment