Header Ads

WAKACHA WATENGANA RASMI


Ile crew ambayo ilikuwa na wasanii waliokubalika sana kwa michano na dress code za ukweli, Wakacha wa B-Hitz Music Group wametengana ambapo baadhi ya memba wameamua kwenda solo. Wakacha ambayo ilikuwa ikundwa na Cyrill, Jux, Gigga Flo, Ricci Boi na Nas 3 sasa imebaki na wasanii watatu baada ya Ricci Boi maarufu kama King Kapita na Nas 3 kujiondoa ndani ya kundi hilo. Habari za uhakika zinadai kwamba wasanii hawa walianza kuwa na tofauti toka wakati wa kufanya video yao ya Here We Go ambapo kutokana na tofauti hizo hiyo video imeshindikana kumalizika.Mpaka haijeleweka kabisa ni tofauti gani zilizopelekea membaz hawa wawili kujitoa. Kwasasa list ya Wakacha inasomeka kama ifuatavyo C.E.O kama kawa ni Cyrill Kamikaze, Jux Vuitton na kiranja wa swagga mtu mzima Gigga Flo

No comments:

Powered by Blogger.