Header Ads

HATIMAYE DIAMOND AMPIGA CHINI WEMA SEPETU


Katika hali isiyo ya kawaida mwanadada Wema Sepetu, JLO wa bongo na mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond wameachana rasmi. Diamond alitamka wazi jana wakati akiongea na waandishi wa habari katika hotel ya Lion iliyopo Sinza. "Washikaji nimewaita hapa nifunguke mbele yenu kuwa nimemwaga rasmi yule demu (Wema) kwasababu hapatani na mama yangu" alisema Diamond ambaye alionekana kumaanisha anachokisema.


Gazeti la burudani la Ijumaa ambalo limeripoti hii habari lilimtafuta Wema ambaye hata hivyo alikataa kuchonga na wanahabari hao na kudai angewatafuta. Uhusiano wa Wema na Diamond ulikuwa kivutio kikubwa kwa wasanii na washabiki wa muziki. Hata hivyo kutokana historia ya mahusiano ya mwanadada mrembo Wema Sepetu wengi walitabiri kutodumu kwa ndoa hiyo. Haya all in all, maisha yanaendelea na tuwaombee tu wasije wakaharibu kazi zao wanazofanya kutokana na kuvunjika kwa uhusiano wao ambao ulikuwa maarufu kupita kiasi.

No comments:

Powered by Blogger.