Header Ads

ALI KIBA NDANI YA MAKAO MAKUU YA WAHINDI


Ali Kiba mzee wa Dushelele kupiga bonge la show pande za wahindi, India. Ali Kiba anategemea kupiga show tatu akiwa kule ambapo show ya kwanza atapiga tarehe 28 October, ya pili 29 October na atamalizia show ya tatu tarehe 30 October. Safari ya Ali K ndani ya India imedhaminiwa na Runner Entertainment.
Akizungumza na KaribuNdani kutokea India, mmoja wa waandaji wa tour hiyo ya Ali Kiba, mtu mzima William maarufu kama Kigje amesema mpango mzima umekamilika na kilichobaki ni utamu tu wa show ambao Ali Kiba ameahidi kuwapa watu wake pande zile.. Runner Entertainment huwa wanashirikiana na Mapesa Ent katika shughuli zao huko nchini India na kwamba wamedhamiria kuleta utofauti katika show hizi. Ali Kiba atapiga show ya kwanza Mysore, ya pili itakuwa Hydrabad na Bangalore..

No comments:

Powered by Blogger.