UDOM WAWAZIDI MAARIFA ASKARI KWA KUFIKA MJINI BILA POLISI KUJUA KUSHTUKIA WANAFUNZI WAKUSANYIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE SQUARE
Wanafunzi Wa Udom Kutoka Vitivo Viwili Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na
Lugha Pamoja Na Kitivo Cha Sayansi Asilia Wakiwa Wamekutana Katika
Viwanja Vya Nyerere Square Baada Ya Kuwazidi Maarifa Polisi
Waliojitahidi Kuwazuia Barabarani Wakati Wanafunzi Walipita Njia Za
Mikato Hadi Kufika Viwanjani hapo
Mwanafunzi Wa UDOM akiwa amebeba Bango ambalo Linasema "Pinda
Adanganya Tena Must Step Down" Mara Baada Ya Kukutana Katika Viwanja Vya
Nyerere Square.
Mwanafunzi Akiwa Amebeba Bango linalosema
"Bila Field (Mafunzo Kwa Vitendo) UDOM ni Shule ya Sekondari" Wakati
wamekusanyika Katika Viwanja Vya Nyerere Square Asubuhi Hii
Wanafunzi Wa Vitivo Viwili Kutoka Chuo KIkuu Cha Dodoma Wakiwa
Wamekusanyika Katika Uwanja Wa Nyerere Square Asubuhi ya Leo Mara baada
ya kuwazidi akili polisi ambao walijipanga kuwazuia wanafunzi hao
barabaranii wakati wanafunzi wakatumia njia za mikato na hatimaye kufika
viwanjani hapo
Wanafunzi Wakimsikiliza Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Mh
Mwakinbinga Wakati Akitoa Maelekezo Jinsi Ya Kuweza kufika Bungeni
Kuonana Na Waziri Mkuu Na Waziri Wa Elimu
Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Akitoa Maelekezo Juu Ya Kufika Bungeni KUonana na Waziri Mkuu
Waandishi Wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali Vya Habari Wakichukua
Habari Wakati Raisi Wa Vitivo hivyo Viwili Wakitoa Maelekezo Muhimu
Wanafunzi Walipokua Wakiimba Nyimbo za Ukombozi Pamoja Na Wimbo Wa Taifa Na Tanzania Tanzania
Maraisi Wa Vitivo Mh Mwakibinga Wa Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha(
Wa Kulia) Na Lema Wa Kitivo Cha Sayansi Asilia Wakiteta Jambo Mara
baada Ya kutoa Maelekezo Kwa Wanafunzi Waliokusanyika Viwanjani hapo
Wanafunzi Wa UDOM wakijiandaa kuelekea Bungeni Wakitokea Viwanja Vya Nyerere Square Asubuhi hii
Vijana Wa IGP Mwema Wakiwa Tayari Nje ya Uzio Wa Nyerere Square
Kwaajili Ya Kuwazuia Wanafunzi Wasifike Maeneo Ya Bunge Lakini Bado
Waliweza Kukubali Kushindwa na Kuzidiwa Maarifa Na Wanazuoni Hao Kwa
Kuzidiwa Maarifa na HAtimaye wanafunzi kuweza Kupita na kukaribia maeneo
ya bunge na hapo ndio mabomu yalipoanzaa kusikika
Askari Polisi Wakiwa Wamejiandaa Kwa ajili Ya kuwazuia Wanafunzi Hao
Lakini Walionyesha kushindwa kete na wanafunzi kukaribia maeneo ya
bunge huku wengi wakiwa wamefika na Hatimaye mabomu kulindima Maeneo ya
Bunge
Kaa Tayari kama Wanavyoonekana hapo wakiwa na shauku ya kupiga
Hatimaye Polisi Wameweza Kukubali kushindwa na Kuzidiwa Kete wakati
wa kuwazuia Wanafunzi Wasiweze kufika Mjini Dodoma Kwaajili Ya Kuelekea
Bungeni Kuonana Na Waziri Mkuu Mh Pinda Kwaajili ya kutoa Malalamiko yao
kuhusu kufutwa Kwa Mafunzo Kwa Vitendo (FIELD) kama Walivyokubaliana
Mwanzo
Hapo Awali wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Asilia Waliweza Kuwahi
Kuamka Na kuelekea Mjini Na Kufanikiwa Kufika Karibu Na Mjini Lakini
Polisi Hao Waliweza Kuwazuia Kwa Muda Lakini Bila Mafanikio Wanafunzi
Waliweza Kugawanyika Makundi na Kupita Njia Tofautitofauti Na Kukutana
Katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere Square kwaajili ya kujipanga upya
Polisi Kwa Kujua Kuwa Waliowazuia Mwanzo Ndo Chuo Kizima Na Kusahau
Au Bila Kujua Kuwa Kuna Kitivo Kingine Kinakuja waliweza kuchanganyikiwa
ni wapi pa kuwazuia wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na
lugha Ambao Walionyesha umahiri wa hali ya juu wa kuweza kupita njia za
mikato hadi kufika mjini pamoja na polisi wachache kuweza kujua
walipopita lakini walishindwa kufika na kupiga bomu moja la machozi
ambalo halikumwasiri mtu yeyote yule
Baada ya Wanafunzi Hao Wa Vitivo Vyote Viwili Kufanikiwa Kufika
Viwanja Vya Nyerere Square Na Kupanga Mikakati kabambe ya Kuelekea
Bungeni Wanafunzi Hao Walianza Kuondoka Na Kuelekea Bungeni Huku Polisi
Wakiwa hawajui cha kufanya kwa kuzidiwa ujanja HAtiamye polisi Waliweza
kuwazuia Wanafunzi Hao Katika Makutano ya Barabara Ya Standi Kwa
Kuwalushia Mabomu ya Machozi Wakati wanafunzi wanakimbilia sehemu
mbalimbali wanafunzi hao waliweza kukutana tena maeneo ya sokoni ambapo
askari waliweza kuwafuata na kupiga mabomu ya machozi ambayo wanafunzi
walionyesha kuwa walijiandaa na kuanza kunawa kwa maji waliyobeba wakati
wakitoka chuo.
Wakati wanafunzi hao Wakiwa Wametawanyika sehemu mbalimbali za Mji Wa
dodoma Wanafunzi waliweza kuharibu bidhaa za watu ambao walikua sokini
wakati wa kukimbia kwaajili ya kunusuru Maisha yao.
Baada ya Dakika Si Zaidi Ya Kumi na Tano Wanafunzi Hao waliweza
kukutana Tena Viwanja Vya Nyerere Square Na Ndipo Mkuu Wa Mkoa Dr
Msekela Kufika Na Kuwaambia Wanafunzi Kuwa Wasubiri Waziri Wa Elimu Mh
Kawambwa Anakuja Kuongea Na wanafunzi Hao.
Muda Zaidi Ya Saa Moja Na Nusu Waziri Wa Elimu Hakutokea Na Hatimaye
Wanafunzi Wakaanza Tena Kuimba Nyimbo za Ukombozi Na Hatimaye polisi
Wakafika Tena Viwanjani hapo Na kuwatawanya Wanafunzi hao.
Mpaka Naingia Mitambo Wanafunzi Waliokamatwa wanafikia 30 huku
wengine wakiachiwa na Mpaka Sasa waliopata majeraha wanakadiriwa kufikia
7 ambapo inasemekana mmoja wa majeraha Hao Amevunjika Mguu Mara baada
ya kupigwa na polisi na Hatimaye kumtelekeza hapo na ndio wananchi wenye
moyo safi kumchukua na Kumpeleka Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma kwaajili
ya matibabu
kwa habari zaidi bofya hapa













No comments:
Post a Comment