BREAKING NEWS:
MAKAMU WA MKUU WA CHUO PROF IDRISA KIKULA ATETA NA WANAFUNZI WA UDOM USIKU HUU
Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa
Kikula Aongea na wanafunzi mbele ya bweni namba tatu kuwaeleza wanafunzi
kuhusu ujumbe aliopewa na serikali.
Katika Hali aliyokuwa akielezea
Ujumbe aliotumwa Na serikali kuwa serikali imesema kuwa wanafunzi
wataenda kufanya mafunzo kwa vitendo na pesa zitaingia kabla ya kuanza
mitihani ya mwisho ambao inatarajiwa kuanzia jumatatu ijayo.
Wanafunzi hao wameonyesha kukataa
ujumbe ulioletwa na Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa Kikula na kuendelea
kushikilia misimamo yao kuwa kesho mgomo uendelee kwa sababu walishawahi
kuahidiwa na Mawaziri Shamsi Vuai Nahodha na Shukuru Kawambwa na Waziri
Mkuu Mh Pinda halafu hakuna kitu na kuchukulia hii ni kama siasa na
ndio maana wanafunzi wamegoma na wamekataa kukubali ombi lililoletwa na
Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa Kikula.
Wakati huo Huo Waziri Mkuu Wa
Serikali ya Wanafunzi Amenusurika Kupigwa Kwa kile kinachosemekana
amewasaliti Wenzao. Mpaka Muda huu hali si shwari UDOM na Hali bado
haijajulikana
Tuendelee Kuvuta Subira Kujua Kama Kesho Mgomo Hupo Au Haupo.
Mchezaji
wa timu ya Simba Mussa Hassan Mgosi akiwa amembeba mchezaji mwenzake
Amri Kiemba mara baada ya kupachika goli la kwanza na la ushindi,
katika goli la timu ya Motema Pembe kutoka DRC kwenye mchezo wa michuano
ya Kombe la Shirikisho la CAF, uliochezwa katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam jioni hii, goli hilo limefungwa kipindi cha kwanza
dakika ya 20 ya mchezo huo mshabuliaji Mgosi aliipokea pasi nzuri kutoka
kwa kiungo Mohamed Banka kufunga goli hilo pekee, hivyo Simba
imefanikiwa kuwatoa "ulimi nje" wapinzani wao Motema Pembe ya DRC.
Mchezaji
Emmanuel Okwi akimtoka beki wa timu ya Motema Pembe katika mchezo wa
Kombe la Shirikisho la CAF katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshika
kibendera akiangalia wakati wachezaji wa timu ya Simba na Motema Pembe
wakichuana katika mchezo wao unaofanyika sasa kwenye uwanja wa Taifa
Credits: Full Shangwe Blogu
Hii ilikuwa jana pale Chang'ombe TCC Club kwenye show
ya GRAND MALT. Wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Chege
& Temba, Chidi Beenz & Chiku K pamoja na Joh
Makini.
Kwa steji ni Joh Makini
Nikiwa mtamboni kwenye show ya Joh
Chidi Beenz na LA Familia
Credits: Bongo Star Link
JUST IN:HATIMAYE UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM) KESHO KUGOMA MARA BAADA YA KUAMBIWA RASMI KUWA HAKUNA MAFUNZO KWA VITENDO
Wanafunzi wa Kitivo Cha Sayansi ya
Jamii, Sanaa na Lugha wakusanyika Mchana huu Kwaajili ya kuamua maswala
mazima ya mafunzo kwa vitendo.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini
maelezo yaliyokua yakitolewa na Raisi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii Mh
Mwakibinga Philipo Juu Ya Mambo yaliyoweza kufanywa na Serikali mpaka
mchana.
Wanafunzi Wa Udom Wakiwa wenye shauku
ya kutaka kujua uamuzi utakaochukuliwa na uongozi wa wanafunzi mchana
huu katika uwanja wa mpira wa kikapu na mbele ya bweni namba tatu
Wanafunzi Wakitawanyika Mara baada ya
Raisi wa kitivo kuwapa uwezo wa kuamua mara baada ya mada iliyotakiwa
kuamuliwa na bunge kuwaa tata na kurudishwa kwa wanafunzi ili iweze
kuamriwa kama katiba ya serikali ya wanafunzi inavyoeleza
Umati wa wanafunzi ukiwa umekusanyika
mbele ya bweni namba tatu na kwenye uwanja wa mpira wa kikapu
wakisikiliza maelezo kutoka kwa Raisi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii
mchana huu
Wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya
Jamii, Sanaa na Lugha wakiendelea kusikiliza kwa makini uamuzi
utakaoamuliwa na wanafunzi wote.
Wanafunzi wakiwa wametawanyika mara baada ya mkutano huo kutawanyika na kufikia maamuzi ya kugoma.
Na Josephat Lukaza - University of Dodoma (UDOM)
Wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma
kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha wamekusanyika mchana huu
mbele ya bweni namba tatu na kwenye uwanja wa mpira wa kikapu kwaajili
ya kumsikiliza raisi wa kitivo cha sayansi ya jamii Mh Mwakibinga
Philipo Kwa ajili y kuelez jinsi ya serikali yake ilivyoweza kufanya
yote yaliyowezekana kufanywa na serikali yake na kuwapa wanafunzi
wenyewe waamue mara baada ya serikali nzima ya wanafunzi kufuatilia
swala hili kwa ngazi husika na kuonekana kuwa hakuna uwezekano wa suluhu
iliyoweza kupatika.
Raisi wa Kitivo Cha sayansi Ya jamii,
sanaa na lugha Ametubia katiba ya serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu
cha dodoma UDOSO kuwapa mamlaka wanafunzi ya kuamua mara baada ya bunge
kushindwa kutoa maamuzi katiba ya UDOSO inasema mada yoyote ile
inayoshindikana kupata suluhu ndani ya kikao cha bunge basi maamuzi
yataammuliwa na wanafunzi Mamlaka hayo ya katiba yamewapa wanafunzi
uwezo wa kuamua pale bunge linaposhindwa kufikia muafaka.
Wanafunzi Wamefikia Muafaka wa Kugoma
hapo kesho Kuanzia Saa Kumi Alfajili Kwaajili ya kwenda bungeni kuonana
na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda Kwaajili ya Kuweza kupata uamuzi juu ya
maswala mazima kuhusu mafunzo kwa vitendo kitu ambacho kiliahidiwa na
Waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa na Waziri Wa Mambo ya Ndani Mh Shamsi
Vuai Nahodha Kuwaahidi wanafunzi wa kitivo hiki kuwa wataenda kufanya
mafunzo kwa vitendo wakati walipofika kusuluhisha mgomo uliotokea tarehe
20 Disemba 2010
Katika Usuluhishii huo Waziri
Kawambwa Na Shamsi Vuai Nahodha Waliweza kuwaagiza uongozi wa chuo na
Tume ya vyuo vikuu Tanzania pamoja na Bodi ya mikopo kufanya mchakato wa
haraka kuwezesha wanafunzi ambao hawana mafunzo kwa vitendo wanakwend
katika likizo ndefu ambayo inatakiwa kuanza mara baada ya wanafunzi
kumaliza mitihani yao ya mwisho wa muhula inayomalizika tarehe mosi
julai 2011
Mgomo Huu Mkubwa Ambao umeweza
kuhusisha baadhi yavyombo vya serikali umekuja mara baada ya Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania Kutoa Tangazo kuwa hakuna kwenda kufanya mafunzo kwa
vitendo kwa kozi ambazo hazina mafunzo kwa vitendo, tangazo hilo
limesababisha wanafunzi, uongozi wa chuo kushangaa uamuzi uliofikiwa na
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Kwa kutoa tangazo hilo wakati walikuaa
wameshakubaliana na Waziri Wa Elimu tayari alishatoa maamuzi.
Habari na www.josephatlukaza.blogspot.com
kwa muendelezo wa habari hizi







No comments:
Post a Comment