Eneo ambalo geti la Lodware ni eneo ambalo lina Nyani wengi. Kwa kipindi
kirefu Nyani hawa wamejijengea tabia ya kukwapua vitu mbalimbali
ambavyo vinaachwa wazi kwenye magari ya wageni au wakati mwingine
kuwapora wageni vitu toka mikononi mwao. Kutokana na ka-tabia haka, mimi
hupenda kuwaita Nyani hawa Mateja, nikiwafaninisha na jamaa wa mitaa ya
huku mijini wanaokwapua simu na vitu vingine kwenye magari.
Mnapolikaribia
geti la Lodware kuna tahadhari za msingi kabisa ambazo inabidi
mzichukue kwa pamoja ili kuepusha tafrani ya namna yoyote na hawa
mateja. Awali ya yote ni kuhakikisha ya kwamba vioo vya magari
vinafungwa na pia roof ya gari inafungwa pia. Mateja hawa hutumia sehemu
hizi kuingia ndani na kuchukua kile kitavutia kwenye mboni za macho
yao.
Baada
ya kufika geti ni vyema kuhakikisha kuwa milango ya magari haiachwi
wazi kwani hiyo ni moja ya njia zao kuingia ndani. Pia, hakikisha mgeni
haubebi kitu chenye muonekano unaofanana na lunch box. Nyani hawa
wanajua kuwa wageni hubeba lunch box kwenye magari na lunch box hizi
huwa na chakula kinachowafaa. hicho ndio kitu cha kwanza huwa wanaanza
kukiandama kwenye magari. Wanapoona mtu (akiwa nje ya gari) kabeba lunch
box au kitu kinachofanan na lunch box, basi mateja hawa hawatasita
kumuandama. Mbaya zaidi ni pale mlengwa wao anapokuwa ni mdada au binti.
Huwa wanawasumbua sana akina dada (bila kujali rangi au utaifa) kama
inavyoonekana katika picha ya kwanza. Pembezoni mwa eneo la kuegeshea
magari, kuna kichaka ambacho mateja hawa huenda kujichimbia na kufaidi
kile wanachokwapua eneo la parking.
Reviewed by
crispaseve
on
7:59 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment