| Gazeti
la Mwanahalisi la leo June 1. 2011 limenukuu yaliyojiri katika kikao
kinachoelezwa kufanyika katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba
jijini Dar es Salaam kati ya viongozi wakuu wa CCM, Katibu Mkuu Wilson
Mukama na Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa. Kikao kilichowahusisha
Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge. Yote
katika yote yaliyoandikwa kuwa yalijiri katika kikao hicho kubwa zaidi
ni maelezo ya majibizano kati ya Lowasa na Pius Msekwa. Na zaidi
maswali matatu ya Lowasa kwa Msekwa. Majibizano hayo yalikuwa hivi.
Msekwa...."Lowasa unatakiwa kujiuzuru nyadhifa zako zote kwenye chama
ili kutekeleza maagizo ya NEC na falsafa ya kujivua gamba". Imeelezwa
kuwa Lowasa alijieleza kirefu juu ya namna asivyohusika na kashfa ya
kampuni ya kufua umeme ya Richmond na namna alivyofanya tukio la
kizalendo kwa maslahi ya Taifa na chama, Tukio la kujiuzuru uwaziri mkuu
na alivyokutana na Rais hivi karibuni. Baada ya maelezo marefu ya
Lowasa, Msekwa alisema... "Lowasa Acha mbio zako za Urais". Lowasa
akajibu kwa upole. "Lini nimetangaza kugombea urais"? Akaongeza swali,
"Lakini hata kama ninataka kufanya hivyo ni haramu kugombea nafasi
hiyo?, Je kuna mliyemundaa?" Maswali haya matatu ya Lowasa kwa Msekwa
yananikanganya sana. Mdau nini tafakari yako juu ya maswali haya na hali
halisi ya kisiasa ya CCM? |
No comments:
Post a Comment