Header Ads

PUSH OBSEVER YAZINDULIWA ASUBUHI YA JANA KEMPISKI HOTEL

Mdau wa akiendelea na kumwaga habari na maelezo zidi juu ya hiyo kampuni mpya ...

Ufuatiliaji wa matangazo kwenye redio na televisheni ulikuwa mgumu kutokana na kukosekana teknolojia ya kisasa ya kufuatilia, watangazaji wakubwa nchini, kama vile makampuni ya simu na vinywaji baridi, wakati mwingine walikuwa wanalipa hata matangazo ambayo hayakurushwa. Lakini kwa ujio wa kampuni ya Push Observer, tatizo hilo litabaki historia. Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, mtangazaji hivi sasa ataweza kufuatilia na kupata repoti ya ambavyo matangazo yake yalirushwa redioni au kwenye televisheni, kwa kuangalia sekunde, dakika, siku na mara ngapi lilirushwa tangazo hilo. Mpango mzima wa uzinduzi umefanyika asubuhi hii Kempinsky Hotel, jijini Dar es salaam. Pichani juu ni Ofisa Mkuu wa Operesheni wa kampuni ya hiyo, Omary Salisbury akielezea namna teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Kwa Habari Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Powered by Blogger.