"DAWA YA MAJI MAHABARA MSITU"
MAELFU KUFURIKA LOLIONDO KUPATA DAWA KWA BABU.
Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya Ngorongoro kata ya Digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine Kupoteza maisha kutokana na msongamano mkubwa wa watu na kuchelewa kupata huduma ya dawa.
Wananchi hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kijiji hicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa muda mrefu. Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani Ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji Mwasapile pia kuna wengine waliofika nyumbani kwa mchungaji huyo na kupata huduma lakini wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri.
Mbali na kuachwa na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu wengi wao wamekuwa wakipata shida ya malazi na chakula kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu wanaowakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda mrefu wengine zaidi ya siku tano na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata chakula kwa shida sana hali ambayo imepelekea hofu kubwa kwani watu wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kuotokana na msongamano huo wa watu .
Pia baadhi ya wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu saba walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.
Mwandishi wa habari hizi mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine wakiwa hawajiwezi kabisa.
Pamoja na kuwa mchungaji Mwasapile alijitahidi sana kuwahudumia wagonjwa hao kwa moyo mkuu, jana jioni ilibidi aongeze wachungaji wengine wawili kumsaidia. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo wagonjwa wanavyozidi kumiminika mahali hapo.
Mchungaji Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu bado na watatoka nchi mbalimbali duniani kufuata huduma hiyo hali ambayo hali ambayo itapelekea mtu kuchukua hata wiki tano kupata huduma.
Mchungaji huyo alisema kuwa yeye Mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi tu na ilipofika mwaka jana Mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.
“Mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu na kweli alikuja mama mmoja wa hapa hawa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza habari za matibabu na watu wengine wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile
Alisema kuwa dawa hii hainyweki mara mbili; tiba yake ni mara moja tu na alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi watapona baada ya siku 21 ambapo alifafanunua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande wa watu wenye Kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo dawa tu.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambukizi mapya kwani hawatapona tena. Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Kwa upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wengeji ambapo alifafanua kuwa awali wenyeji walikuwa wanadharau dawa hiyo na kusema kuwa hawamwamini lakini baada ya kuona wageni wengi wanajitokeza kuja kunywa dawa hiyo ndio na wao wameanza kujitokeza kwa wingi.
Pia alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa wao kujitahidi kuwaleta wagonjwa wao wakiwa angalau wana nafuu kiasi na wasiwachukue wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa hivi msongamano wa watu ni mkubwa hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumiwa .
”Unajua napenda kuwaambia wasiwachukue wagonjwa wao wakiwa mahututi kwani ndo inaweza kuwasababishia madhara. Wanapokuja wanakuta kuna wagonjwa wengine hivyo unakuta inachukuwa muda kuhudumiwa kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kupoteza maisha akisubiria huduma na kama watakuwa wamewachukua hospitalini basi wabebe dawa ambazo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
Pia gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa wakiwa wanauza shilingi 2000.
Alisema kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipato kila siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Juma alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifika Ngorongoro akiwa anaumwa na amebebwa lakini tangu anywe dawa hiyo amesisimama mwenyewe na anatembea kitu ambacho amemshukuru Mungu kwa kumleta mtumishi huyu katika nchi ya Tanzania
Baadhi ya wagonjwa ambao waliohudhuria katika kijiji hicho waliomba jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza ghasia ambao wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili kuweza kusaidia vurugu zisitokee.
Walisema kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.
DAWA IPO.....KUIPATA SHUGHULII.........FOLENI... YA HATARI.

No comments:
Post a Comment