LAYD JD ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT NA KUJIONEA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA GONJWA HATARI LA FISTULA
FISTULA ni ugonjwa hatari unaowapata
wasichana na wanawake wakati wa kujifungua.Wasichana/Wanawake wanao ishi katika
mazingira duni na ya kimaskini wanajikuta wanalazimika kujifungulia
majumbani mwao wakisaidiwa na wakunga badala ya kwenda Clinic za Wazazi.
Jambo linalopelekea wanapatwa na ugumu
wakati wa kujifungua na kusababisha kupatikana kwa ugonjwa wa Fistula.
Madhara
ya Fistula ni msichana/mwanamke kupatwa na haja ndogo au haja kubwa
bila kujijua na hali hii huwatokea mara kwa mara na hawawezi kujizuia.
Mwanamke alie na Fistula hulazimika
kuacha kazi au kwa familia zisizo elewa hutokea pia kutengwa na watu wa
karibu kutokana na kuwa na harufu ya kutokwa haja mara kwa mara hata
mbele za watu bila kujijua.
Kwa wastani wasichana/wanawake milioni 2 Africa na Asia ya kusini
wanaishi na Fistula.
FISTULA INATIBIKA
Na cha kufurahisha zaidi CCBRT inatoa
matibabu ya ugonjwa huo bure.
Kama una mtu yoyote unamfahamu ana
tatizo hili hata kama hana hela ya usafiri kutoka popote alipo, iwe
mjini au kijijini hapa nchini Tanzania.
Tafadhali chukua jukumu la kuwasiliana
na CCBRT au hata mimi ili tuweze kuokoa maisha ya mwanamke.
CCBRT iko tayari kumgharamia afike
Hospital na atapata matibabu bure pamoja na huduma zote za msingi kama
chakula na malazi.
Na akishapona pia atapatiwa usafiri wa kurudi popote
alipotokea.
No comments:
Post a Comment