Mfalme Mswati III Abadili Jina la Nchi Yake
MFALME
Mswati wa III wa Swaziland amebadilisha jina rasmi la taifa hilo kutoka
Swaziland na kuliita Ufalme wa eSwatini (The Kingdom of Swaziland) wakati
wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 50 na
wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.
Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana
ya ardhi ya Waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa III kwa miaka
mingi. eSwati ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia
katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 na katika ufunguzi wa
bunge la nchini mwake mwaka 2014.
Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki na ametawala tangu mwaka 1986.
Mswati III kwa sasa ana wake 15 akiwa
anaifuata rekodi ya Baba yake aliyekuwa na wake 125. Wanaharakati wa
kutetea usawa wa jinsia wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa
kushangaza na unawabagua wanawake.
Mswati III ametoa sababu kuu ya
kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aendapo katika mikutano ya
kimataifa, mataifa mengine wamekuwa wakilichanganya taifa lake na nchi
ya Switzerland.
Nao raia wametoa maoni yao juu ya hatua
ya mfalme wao na kusema kuwa badala ya kushughulika na jina la nchi
yake, badala yake alipaswa kupasua kichwa ni namna gani anaweza
kuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaodidimia siku hadi siku.
Kwa taarifa yako, Mfalme Mswati
anajulikana pia kama Ngwenyama kwa lugha ya taifa hilo jina likiwa na
maana ya ‘Simba’, lakini pia anajulikana ullimwenguni kwa tabia yake ya
kuoa wake wengi na kwa kuzingatia mavazi ya jadi pamoja na kuthamini
mila na desturi.
No comments:
Post a Comment