BUNGENI: KAULI RASMI YA SERIKALI KUHUSU TRILIONI 1.5 – VIDEO
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema hakuna fedha taslimu kiasi cha shilingi trilioni 1.51 iliyopotea au kutumika kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge.
Kijaji amesema madai ya baadhi ya watu kuhusu fedha hizo hayana msingi wala mantiki yeyote kwa kuwa hawalitaki mema taifa na serikali ya awamu ya tano.
Aidha, Kijaji amesema utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.
Jana, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Omary Mgumba alimtaka Waziri wa Fedha na Mipango (kwa niaba ya serikali) kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotevu wa Trilioni 1.5 ambazo zinadaiwa kutofahamika matumizi yake kwa mujibu wa ripoti ya CAG.
No comments:
Post a Comment