Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua mkutano mkuu wa BAKWATA mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
Mufti
wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry akiongea kabla ya kumwalika
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kufungua mkutano mkuu wa BAKWATA
kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akihutubia wakati anafungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na wajumbe baada ya kufungua mkutano
mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akilakiwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary
bin Zubeiry alipowasili kufungua mkutano mkuu wa BAKWATA kwenye ukumbi
wa Msekwa mjini Dodoma.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 31, 2018) kwenye Mkutano
Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) uliofanyika katika
ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu
wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo.
“Dini
ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali
inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa
katika amani ya nchi yetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde
amani yetu”
Waziri
Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa sana kwa binadamu na
ndio maana wote wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au
kikundi chochote kujaribu kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea
kuwaunganisha waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao au
madhehebu yao.
Waziri
Mkuu amesema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye
ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote amekuwa akisisitiza jambo
hilo na kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo
chao.
“Ni
muhimu sana kwa ninyi wasaidizi wa Mufti mlio kusanyika hapa
muhakikishe mnalisimamia hili katika maeneo yenu. Katika hili napenda
kuwahakikishia kuwa Serikali yenu iko pamoja Mheshimiwa Mufti kutekeleza
nia hiyo njema.”
Amesema
ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ni kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari
kusikiliza maoni, ushauri na mapendekezo yeyote kutoka kwa viongozi wa
dini . ‘Milango iko wazi saa zote ‘
Ameongeza
kuwa yeye si mtaalamu sana kama walivyo Masheikh hao lakini anakumbuka
maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani sura Al Imran aya ya 103
yanayosema “ Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala
msifarakane”
Mkutano
huo umehudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Mufti wa Tanzania Sheikh Zubeir,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wajumbe wa Baraza la Ulamaa,
Masheikh na viongozi wa BAKWATA wa mikoa na wilaya zote Tanzania.
No comments:
Post a Comment