TAARIFA YA DC HAPI KUMTEMBELEA MSANII MAN DOJO ALIYEBOMOLEWA NYUMBA YAKE
Leo
asubuhi nimefika alipokua akiishi msanii Man Dojo.Taarifa ya awali
inaonesha kuwa eneo alilojenga kuna viwanja vitatu ambavyo vina hati na
kuna watu walipewa mwaka 2003.Mwaka 2013 viwanja hivyo vikiwa
havijaendelezwa,Man Dojo aliuziwa na mtu aliyedai ni mmiliki wa eneo
hilo kwa Tsh milioni 3 wakimuaminisha kuwa ni mali yao.
Wenye hati wameeleza kuwa walifungua kesi na kushinda katika Baraza la ardhi la wilaya, hivyo kupata amri ya kubomoa.Baada ya yake kubomolewa, kwa sasa Man Dojo na familia yake wanalala nje.
Baada ya kuona na kusikiliza mechukua hatua zifuatazo kwa awali:-
1. Nimeelekeza Man Dojo atafute nyumba ya kujistiri yeye na mkewe eneo la Mbweni kwa kipindi cha mpito ambayo nitamlipia kwa miezi sita.
2. Nimeagiza wote waalioshiriki kumtapeli Man Dojo kwa kumuuzia kiwanja huku wakijua si mali yao wakamatwe na jeshi la Polisi haraka iwezekanavyo.Kitendo walichofanya ni jinai na lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
3. Nimemuita Man Dojo ofisini kwangu siku ya jumanne saa 4 asubuhi na wenzie ambako tutafanya kikao na mashauriano na wataalam wa ardhi wa manispaa na uongozi wa kata ya Mbweni ili kujiridhisha kiini cha jambo hili, kupitia nyaraka zote na kuona namna tutakavyomsaidia kwa kutumia HEKIMA, BUSARA NA UBINADAMU.
4. Nimeagiza, Mkurugenzi kupitia idara ya ardhi na Mipangomiji Kinondoni kuniletea taarifa ya watu wote waliopewa viwanja kwa kuanzia na Mbweni ambao hawajaendeleza viwanja vyao hadi sasa (kama masharti ya hati yanavyowataka).
Kutoendeleza viwanja kunatoa mwanya kwa matapeli kuwatapeli wananchi wenye shida ya dhati ya ardhi ya kujenga makazi kama ilivyokua kwa ndugu yetu.Wako watu walipewa viwanja mwaka 2003 lakini hadi leo wameshindwa kusafisha na kuendeleza viwanja vyao.Badala yake viwanja hivyo vimekua vichaka na maficho ya wahalifu.
5. Siku ya jumatano wiki ijayo nitazungumza na umma juu ya nini kimejiri katika kikao changu cha jumanne na namna gani tutamsaidia na kumshauri Man Dojo.Nafahamu jinsi ilivyo taabu kujenga, nafahamu jinsi kazi ya sanaa ilivyo ngumu hadi kudunduliza na kujenga.

Lakini nawaasa wananchi wote wa Kinondoni kuchukua tahadhari na kujiridhisha kabla ya kufanya manunuzi yoyote ya kiwanja.Ni vyema kupata ushauri kwa wataalam wetu wa ardhi kabla ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi.
Msanii
Man Dojo akielezea jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi
sambamba na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa serikali
ya mtaa wa Mbweni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi akimsikiliza Msani Man Dojo akielezea namba tukio la nyumba yake lilivyokuwa,mapema leo jijini Dar
No comments:
Post a Comment