MATUMIZI YA KIKOA CHA DOT TZ NA DOT AFRIKA KUKUZA UCHUMI WA AFRIKA
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
Watanzania
washauriwa kusajili na kutumia kikoa cha dot tz (.tz) na dot Africa
(.africa) katika matumizi ya intanenti kwa ajili ya kutoa utambulisho wa
kitaifa, ki-bara na kukuza uchumi wa Taifa na Bara la Afrika.
Akizungumza
leo Mjini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Registry.Afrika Lucky Masilela
amesema kuwa vikoa hivyo vinafaida mbalimbali ikiwemo kupunguza gharama
za mawasiliano na pia kukuza uchumi wa nchi na bara zima la Afrika
kutokana na fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi
na bara husika.
“Nitoe
ombi kwa wale wote wanaotumia mtandao watumie mtandao wa dot tz au dot
Afrika kwa sababu vikoa vingine haviwezi kusaidia Afrika, kutokana na
fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi husika”
ameongeza Masilela.
Aidha,
Masilela amefafanua kuwa Umoja wa Afrika (AU) uliridhia maombi ya
rajisi ya dot africa kufanya kampeni ya matumizi ya kikoa cha dot
Africa, ambapo Rajisi ya dot africa iliainisha maeneo matano (5) ya
kufanya kampeni hiyo kwa niaba ya bara lote la Afrika. Maeneo hayo ni
Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kaskazini, Afrika ya kati, Afrika
Magharibi na Afrika ya kusini.
“Lengo
kuu la kampeni hii ni kuwahamasisha waafrika wote watumie kikoa cha dot
africa na pia kujenga hamasa ya waafrika kujivunia uafrika wao na
kujenga uchumi unaotegemea rasilimali ya kikoa hiki pekee kinacho
watambulisha na kuwaunganisha waafrika wote” ameongeza Masilela.
Vile
vile amesema kuwa kampeni hiyo inaudhihirishia ulimwengu kuwa
ucheleweshwaji wa rasilimali pekee ya kuwatambulisha waafrika wote
kwenye mtandao wa Intaneti umefikia hatima yake hivyo Waafrika sasa, kwa
kutumia kikoa cha dot africa wanauwezo wa kuwasiliana, kutoa huduma,
kufanya biashara (taasisi za umma na binafsi) bila bugudha yoyote katika
mtandao wa Intaneti.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network Information Centre
Mhandisi Abibu Ntahigiye amesema kuwa rajisi ya dot africa (ZACR)
ilipewa mamlaka ya kuendesha rajisi ya dot africa mwezi Februari 2017
ikiwa ni baada ya miaka mitano (5) ya juhudi za kutafuta uhalali wa
kufanya hivyo.
“Kufuatia
mafanikio hayo, timu ya dot africa ilipewa jukumu na Umoja wa Africa
(Africa Union - AU) kuendesha kampeni za kuhamasisha matumizi ya kikoa
cha dot africa barani kote kwa kipindi cha miezi sita (6) kuanzia Agosti
2017 mpaka Januari 2018” ameongeza.
Naye
Mwanasheria wa Rajisi ya Tanzania (.tz) Sarah Mhamilawa amesema
matumizi ya dot tz ni rahisi na panapotokea tatizo la kiufundi muhusika
anapiga simu .tz na tatizo hutatuliwa papohapo tofauti na vikoa vingine
ambavyo huhitaji kufuata mlolongo uliowekwa kwa ajili ya utatuzi wa
tatizo husika ambao huchukua muda kutatuliwa.
Kampeni
ya matumizi ya dot africa imeambatana na kuendesha magari (roadshow)
wakiwa na Bendera ya dot africa kutoka Afrika Kusini ambapo safari
ilianza Januari 1, 2017 kuelekea Addis ababa, Ethiopia kupitia Botswana,
Zimbabwe, Zambia, Tanzania na Kenya.
Aidha
timu hiyo ikiwa Tanzania imeanzia kampeni hiyo Tunduma kupitia Iringa,
Dodoma, Arusha na Kilimanjaro ambapo wakiwa Kilimanjaro watapandisha
bendera ya dot Africa na dot tz kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre
Mhandisi Abibu R. Ntahigiye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara
(Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa
kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani
Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya
Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky
Masilela(wakwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow
Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha
matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network
Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye na mmoja wa wajumbe wa
msafara huo Ndg. Ronald Schwaerzler
Mmoja
wa wajumbe wa msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign)
inayofanywa na taasisi za mitandao ya intaneti za Dot tz na Dot africa
kuhamasisha matumizi ya mitandao kwa Afrika Ndg. Ronald Schwaerzler
(wapili kulia) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu ratiba ya kupanda mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kampeni hiyo
leo mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya
Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela na wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R.
Ntahigiye
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dododma Ndg. Jabera Matogolo(wakwanza kulia)
akielezea namna ambavyo mtandao wa intaneti unavyosaidia kukuza
kiswahili wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya
msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi
ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya
intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma.
ashiriki
wa kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign)
inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya
mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walipokutana na waandishi wa habari
leo mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment