TOSAMAGANGA ALUMNI ASSOCIATION WATUMIA ZAIDI YA MILLION 30 KUJENGA CHOO BORA KATIKA SHULE SEKONDARI YA TOSAMAGANGA WALIOSOMA.
Mkuu wa shule ya
sekondari Tosamaganga Iringa Damas Mgimwa akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mwenyekiti
wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za
kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi
wakati wa kukata utepe wa kufngua choo hicho
Mwenyekiti
wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za
kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi
akiwa na mgeni rasmi wa hafla
hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa wakikagua ubora wa vyumba vya vyoo hivyo
Hili ndio jengo jipya la choo kipya kilichojengwa na Tosamaganga Alumni Association kwa gharama ya shilingi millioni 30
Hawa ni baadhi ya wanafunzi
waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya
Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo
la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo.
Na Fredy Mgunda.
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.
Na Fredy Mgunda.
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.
akizungumza
wakati wa hafla ya kukadhi choo hiyo mwenyekiti wa kamati ya
Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha
(ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa
lengo ni kukikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati
shule hiyo kutokana na miundombinu ya sasa si rafiki kwa wanafunzi.
"Maendeleo
niliyopata mimi ni kutokana na kupata elimu katika shule ya Tosamaganga
hivyo lazima tuikumbuke kwa kuendelea kuipatia msaada kadili
tunavyoweza maana ukituangalia hapa unatuona wote tunavipato vizuri
hivyo ni budi kukumbuka wapi tumetoka na tulikotoka kupoje tujia hivyo
tutaithimini hii shule kila wakati kama tulivyofanya hivi sasa" alisema
Mbilinyi
Mbilinyi
aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha
upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.
“Leo
nimerudi katika shule hii ya Tosamaganga kuja kusaidia kutatua
changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii
inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi tumeanza kwa kujenga
choo lakini changamoto bado zipo nyingi" alisema Mbilinyi
kwa
upande wake mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio
mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa aliwataka
wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya hiyo wawe
vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali kurudisha
fadhila katika shule hiyo.
"Nimekuwa
nikipiga kelele muda mrefu kwenye vyombo vya habari muda mrefu juu ya
kuzijali hizi shule zilizotuletea mafanikio ila saizi naanza kuona
matumaini ya wanafunzi wengi wanazikumbuka shule walizosoma hapo awali
ni jambo kubwa na la faraja sana" alisema Masunya
Masunya
alisema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na
wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau
wote kuzikumbuka shule walizosoma.
“Wafanyakazi
na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya
shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania”
Alisema Masunya
Naye
Wakili msomi Protas Ishengoma aliwaomba wanafunzi mbalimbali waliosoma
katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio
chanzo cha mafanikio yao ya leo.
“Hebu
angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado
ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili
kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka
shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa
nchini wote wamesoma katika shule hii”.alisema Ishengoma
Shule
ya Tosamaganga ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali
katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa
maisha sasa kwanini leo hii hawazi kumbuki.
katika
mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe
zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba
serikali kuharakisha utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment