RAIS DKT MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU YA KIKAZI MKOANI KIGOMA.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
RAIS
Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuanza ziara ya siku tatu ya kikazi
Mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine atazindua barabara zenye
kiwango cha lami na mradi wa maji.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa Rais atawasili mkoani Kigoma
kupitia Wilaya ya Kakonko tarehe July 21 akitokea Mkoani Kagera ambapo
atafanya uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutokea
Nyakanazi hadi Kibondo yenye kilometa 50.
Mkuu
wa Mkoa alisema pia siku hiyo Rais atafanya mkutano wa hadhara na
wananchi katika Wilaya ya Kakonko ili kusikiliza kero zao mbali
mbali,pia Rais ataelekea Wilayani Kasulu ambapo pia atazindua barabara
kidahwe mpaka kasulu iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa
kilometa 63.
Maganga
alisema July 22 Rais ataweka jiwe la msingi mradi wa maji uliopo
Manispaa ya Kigoma Ujiji na kisha atafanya mkutano wa hadhara na
wananchi katika uwanja wa Lake Tanganyika.
Na
July 23 Rais ataelekea Wilayani Uvinza kwaajili ya kuweka jiwe la msingi
kwenye mradi wa maji uliopo katika Kata ya Nguruka eneo la amani na
baadae mkutano wa hadhara na wananchi.
Maganga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais kwani hii ni ziara yake ya kwanza tokea uchaguzi Mkuu ufanyike.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli Mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment