EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA
Na Editha Karlo -Globu ya jamii-Kigoma
SHIRIKA
la Kimataifa lisilo la kiserikali la EngenderHealth limetoa msaada wa
vifaa tiba chini ya ufadhili wa Bloomberg kwa Mkoa wa Kigoma ili
kuboresha huduma za afya ya uzazi.
Akiongea
wakati wakukabidhi vifaa hivyo muwakilishi wa shirika la EngenderHealth
kutoka makao makuu Dar es Salaam Dkt.Godson Maro alisema kuwa lengo lao
ni kuendelea kuboresha huduma za uzazi,ikiwa ni sambamba na kupunguza
vifo vya mama na mtoto.
Dkt
Maro alivitaja vifaa walivyotoa msaada kuwa ni pamoja na vitanda vya
kujifungulia,mashine za kupima mapigo ya moyo ya mtoto,mzani wa kupima
uzito,vitanda vya kupumzikia akina mama baada ya kujifungu,mashine ya
kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni na drip stand vyote vina
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 374.
"Vifaa
hivi vitapelekwa katika zahanati mbalimbali zilizopo Mkoani hapa zenye
upungufu wa vifaa tiba pia tutaendelea kushirikiana na serekali
kuboresha huduma za afya ili kufikia malengo makubwa ya kupunguza vifo
vya mama na mtoto"alisema
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alishukuru kwa msaada huo wa
vifaa tiba kwani utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa
wanakutana nazo katika utoaji wa huduma.
Dkt Chawote alisema kuwa vifaa hivyo watavitunza vizuri ili visaidie wananchi wengi na kudumu kwa muda mrefu.
Alisema
Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya watumishi katika zahanati nyingi na
sababu kubwa ni mbiundombinu hasa ya. barabara hali inayofanya watumishi
wengi wakipangiwa kazi huwa hawafiki.
Muwakilishi wa shirika la kimataifa lisilo la kiserekali la EngenderHealth Dkt Godson Maro kutoka makao makuu Dar es Salaam akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote vifaa tiba vilivyotolewa na shirika hilo ili kuboresha huduma ya uzazi kwa mama na mtoto
Kikosi cha wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserekali la kimataifa la EngenderHealth kutoka Dar es salaam na Kigomawakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhino ya vifaa tiba.
No comments:
Post a Comment