Airtel na GSMA wandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi
Kampuni
ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa
mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi
ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.
Mashindano
hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na
muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha
washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya,
Uganda na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo makuu
matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya
jumla (bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel
yaani ( Airtel Comviva mobile wallet).
Tanzania
imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama
kiongozi katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga
mifumo ya malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa ya
kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za
mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel
Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni muhimu kwa vile
unawezesha wajasiriamali wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo itaweza
kusaidia kufanya malipo kupitia simu za mkononi kwa haraka na hivyo
kuokoa kupoteza muda kupanga foleni kusubiria kufanya malipo.
Sisi
Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele kuwezesha wajasiriamali kwa
njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano tunaendeleza uwezeshaji huo
kwani kwa kila suluhu itakayopatikana haitaishia hapa mbali itaendelea
kuboresha na kuwekwa kwenye mfumo wa malipo ya simu za mkononi, alisema
Nchunda.
Kwa
upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA Gareth Pateman alisema
washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhi moja au mbili
katika zile tatu huku mshindi akipata ticketi ya kwenda Barcelona, Spain
huku akiwa amelipiwa gharama zote.
Mkuu
wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa
washiriki kutoka Tanzania wakati mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo
ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na
Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi
ulimwenguni GSMA.
Mkuu
wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa
washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia
simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva
wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni
GSMA
Mkuu
wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa
washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia
simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva
wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni
GSMA
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana baada ya ufunguzi wa
mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi
yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa
mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.
No comments:
Post a Comment