RUFAA DHIDI YA MBUNGE WA BUNDA MJINI ESTER BULAYA YATIMBA MAHAKAMA YA RUFAA JIJIJI DARES SALAAM
Aliyekuwa
kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira akiwa katika
jengo la Mahakama ya Rufaa jijiji Dares Salaam akizungumza jambo na
baadhi ya mawakili kabla ya kusikiliza kwa Rufaa ya kesi yake dhidi ya
Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya. Katika kesi hiyo jopo la majaji
watatu wa Mahakama ya Rufaa limepanga kuendelea na kesi hiyo Jumatatu
ijayo ya Aprili 15, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa leo Aprili 11,
mwaka huu katika Mahakama hiyo baada ya Pande zote mbili kutoa
maelezo ya sababu za rufaa.
Wakili
wa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Tundu Lissu akizungumza jambo na
mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na
wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga hukumu ya Mahakama Kuu
Kanda ya Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.
Wakili
Constantine Mutalemwa akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa
habari mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa
lilifunguliwa na wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga hukumu ya
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo,
Ester Bulaya.(PICHA NA MAGRETH KINABO)
No comments:
Post a Comment