PROFESA MUHONGO AKUTANA NA WENYE NIA KUWEKEZA SEKTA YA NISHATI NCHINI
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akimsikiliza
mwekezaji kutoka Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta (kulia). Katikati ni
Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya umma katika Benki ya
Stanbic, Noella Kimaro, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Thomas Buonga na Mbunge
wa Sumbawanga, Aeshi Hillary, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), walipomtembelea ofisini kwake Dodoma hivi
karibuni na kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiagana na Ujumbe
kutoka Benki ya Stanbic, waliofika ofisini kwake mjini Dodoma, kueleza nia yao
ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. Kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa
Sumbawanga, Aeshi Hillary.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo
wakati wa kikao baina yake na mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer (katikati),
aliyemtembelea ofisini kwake Dodoma hivi karibuni na kueleza nia ya kuwekeza
kwenye sekta ya nishati nchini. Kulia ni Ofisa kutoka Ubalozi wa nchi hiyo,
Derrick Katunzi.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwa katika picha
ya pamoja na mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer (kushoto) na Ofisa kutoka
Ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi (kulia).
Na Veronica Simba - Dodoma
Wawekezaji mbalimbali wamemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ofisini kwake mjini Dodoma na kumweleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali katika sekta ya nishati nchini.
Akizungumza na Waziri Muhongo, mwakilishi wa Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta aliwasilisha nia ya Kampuni hiyo ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Thomas Buonga akiwa ameambatana na Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya Umma wa Benki hiyo, Noella Kimaro, walimweleza Waziri kuwa wanaangalia fursa ya kuwekeza katika miradi ya sekta ya nishati.
Naye, mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer, akiwa amefuatana na Ofisa kutoka ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi, alisema nia ya kampuni yake ni kuwekeza katika sekta ya nishati hususan uzalishaji wa umeme kwa kutumia upepo.
Waziri Muhongo aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia kupata ushirikiano kutoka serikalini endapo watakidhi vigezo stahiki vya uwekezaji vilivyowekwa.
No comments:
Post a Comment