Benki ya KCB Tanzania yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali Mkoa wa Arusha.
Meneja
wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea
na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali
yaliyotolewa na benki hyo mkoani Arusha.
Afisa
Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake
wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na
benki hiyo mkoani Arusha.
Mwalimu
wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC)
Nina Nchimbi akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya
KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Arusha.
Meneja
wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa
wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali
waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki
hiyo katika mkoa wa Arusha.
Katika
swala zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania
inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali
yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke
mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake
ishindwe kuendelea.
Benki
ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya
Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar ambapo matawi
ya benki hiyo yapo.
Mafunzo
haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na
yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za
kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework),
Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za
kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi
ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao
maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao.
Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
No comments:
Post a Comment