ZIARA YA MAKONDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KINONDONI YANOGA LEO, AKATIZA VICHOCHORO KUSAKA KERO, ACHAPA KAZI KIKAMILIFU NA AFANDE SIRRO, AMTUMBUA MGANGA MKUU
TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam, leo. Zifuatazo ni taswira katika picha kama alivyowanasa Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo aliyekuwa katika ziara hiyo.
TANDALE
🔻
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha
Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa
katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula
Makonda
na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za
wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam,
Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro.
Salum
Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa
jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese
Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kieyeji aliowakuta katika kwenye kilabu cha pombe hizo, eneo la Uwanja wa Fisi
Jamaa
aliyejitambulisha kwa jina la Mandela akikata funda la pombe ya
kienyeji mbele ya Makonda bila wasiwasi kuwa yupo na Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam
Makonda
akijaribu kupiga hodi kwenye moja vya vyumba inayoelezwa kuwa ni ya
madanguro ya ukahaba katika eneo hilo la Uwanja wa Fisi. Pamoja naye ni
Hapi na Sirro
Kamanda
Sirro naye akijaribu kumsaidia Makonda kupisha hodi lakini pia bila
mafanikio ya kuitikiwa na waliokuwa wamejifungia ndani
Makonda akichukua bia kutoka kwa mhudumu wa baa pekee aliyoikuta wazi wakati myinge zote zikiwa zimefungwa kuhofia ujio wake.
Makonda
akiitazama kwa makini bia hiyo kuona tarehe yake ya mwisho wa matumizi,
ili kujiridhisha kwa kuwa huelezwa kwamba baa zilizopo eneo hilo la
Uwanja wa Fisi huuza vinywaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi.
Bia hiyo aliikuta bado inafaa kwa matumizi.
SHULE
Makonda
akitazama paa la chumba cha darasa katika shule ya Msingi Tandale,
lililoporomoka wakati wa upepo mkali ulioambatana na mvua
MIUNDOMBINU YA BARABARA
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama majitaka yakitiririka
kwenye daraja la barabara kutoka Tandale kwenda Mwananyamala. Makonda
aliahidi barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami, la kwamba kabla ya
hatua hiyo itafanyiwa matengenezo ya awali kuziba makorogoro ili iweze
kupitika.
Makonda akipita pembeni pembeni kukwema maji machafu yaliyotuama kwenye sehemu ya barabara hiyo
Mara huyu mama naye akamvaa na kumweleza kero zake wakati akipita
MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE
MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi akimkaribisha Makonda kuanza
kuunguruma ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu papo hapo
au baadae, katika mkutano wa hadhara uliofayika kwenye Viwanja vya
Shule ya Msingi Tandale, leo
Makonda akizungumza
Makonda akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.
Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifuatilia jambo kwenye simu
yake wakati wa mkutano huo. Mpogolo ni miongoni mwa waratibu wa ziara
hiyo ya siku kumi ya Makonda katika wilaya zote za mkoa wa Dar es
Salaam.
Watu wa huduma ya kwanza wakimpeleka kwenye gari ili kupelekwa haraka hospitali baada ya kuangua wakati wa mkutano huo
Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa la Manispaa ya Kinondoni
Wananchi kwenye mkutano huo
Makonda akianza kujibu kero kwa kuwahoji watendaji kulingana na wananchi walivyotaka kujibiwa kero husika.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya (aliyeshika kinasa sauti),
akisubiri hukumu ya Makonda baada ya kushindwa kueleza ikiwa alikuwa
anajua au hajui kadhia ya dawa kuibwa mara kwa mara katika Zahanati ya
Tandale kama wananchi walivyolalamika, ambapo alisema hajui
"
Haiwezekani uwe Mganga Mkuu wa Wilaya katika mkoa wangu halafu hujui
kuhusu kuibwa kwa dawa kwenye zahanati, hii haikubaliki, kuanzia sasa si
mganga Mkuu wa Kinondoni, Nitawaambia wizara inayokuhusu wakupangine
wilaya katika mikoa mingine ambako watavumilia uzembe kama papo",
alisema Makonda wakati akimtumbua Msuya kwenye mkutano huo wa hadhara
uliofanyika shule ya Msingi Tandale. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-
theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment