PLUIJM, LWANDAMINA KIROHO SAFI WATAMBULISHWA RASMI LEO
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAKAMU
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemtambulisha rasmi kocha
mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina, aliyechukua nafasi ya
Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyevikwa viatu vya Mkurugenzi wa ufundi
wa timu hiyo.
Lwandamina
anachukua mikoba ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyebadilishiwa
majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi ili kumsaidia Mzambia huyo katika
masuala mbali mbali ya maendeleo ya klabu hiyo, na moja kwa moja Mzambia
huyo huku mzambia huyo akafunguka juu ya kikosi atakachoingia nacho
vitani.
Sanga
ameweka wazi kuwa ujio wa kocha huyo sasa ni rasmi na wamempa kandarasi
ya miaka miwili,lengo kubwa ikiwa ni kuongeza nguvu kwenye kikosi cha
wanajangwani hao katika kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom na
michuano ya kimataifa.
"Uongozi
wa Yanga leo hii unayo furaha kuwatambulisha kocha mkuu George
Lwandamina na Mkurugenzi wa ufundi Hans Van De Pluijm, tunaamini kwa
pamoja wataweza kuipa mafanikio zaidi timu yetu kutoka hapa ilipo na
kusonga mbele zaidi" amesema Sanga.
Baada
ya utambulisho huo, Kocha mkuu Lwandamina akafunguka na kusema kuwa ni
changamoto mpya kwake kwani anajua Yanga ni klabu kubwa na amepewa
nafasi hiyo na kwa kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla na
wachezaji kwa pamoja atahakikisha anatumia kila kinachowezekana
kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi
klabu Bingwa Afrika.
Akaeleza
kuwa kuna habari zinazoenea kuwa anakuja na wachezaji wapya kutoka
Zesco, akasisitiza zaidi kuwa "Nasikia tetesi kuhusu wachezaji wapya
kutoka Zesco kusajiliwa Yanga mimi kama kocha mkuu sijui chochote labda
michakato hiyo inafanyika bila mimi kushirikishwa kikosi kilichopo
ndicho nitaendelea nacho".
Mkurugenzi
wa ufundi wa klabu hiyo Pluijm akawa na yake ya kusema na kueleza kuwa
hana shida na kubadilishiwa majukumu na zaidi ataendelea kushirikiana na
benchi la ufundi kwa ujumla katika kuhakikisha wanaendelea kutetea
ubingwa wao na kufanya vizuri kwenye kombe la Klabu Bingwa Afrika.
Makamu
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akimkabidhi jezi ya timu
hiyo Kocha Mkuu George Lwandamina leo Jijini Dar es salaam.
Kocha
Mkuu George Lwandamina akisalimiana Mkurugenzi wa benchi la Ufundi Hans
Van De Pluijm ambaye awali alikuwa ndiye kocha Mkuu.
Makamu
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa utambulisho wa kocha mkuu Mzambia George Lwandamina
(kulia) pamoja na nafasi ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyechukua
nafasi ya mkurugenzi wa ufundi.
No comments:
Post a Comment