ATI KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 1.2 KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI
Wakala
wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) umeitaka serikali ya Tanzania
kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake ili kuwekeza dola za Marekani
bilioni 1.2 (2.6tr/-) katika sekta ya nishati utakaoongeza megawati
1,200 katika gridi ya taifa.
Tanzania
ni mmoja wa wajumbe waliasisi ATI wakala ambao ulianzishwa ili kutoa
bima kwa wawekezaji pamoja na kufanya shughuli nyingine za kibiashara
miongoni mwa nchi za Afrika ambazo ni wanachama. Chini ya ubia ambao
ulisainiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa mwaka
2001, Tanzania na nchi nyingine zilikubaliana kutoa upendeleo wa kupata
mkopo katika miradi yote inayoungwea mkono na ATI.
Ahadi
hiyo ambayo inatoa uhakika kwa nchi mwanachama ambao utaiepusha na
madai yoyote katika miradi inayoungwa mkono na ATI, kuwapatia
wawekezaji, wagavi na na nafasi nyingine muhimu katika kuzindua miradi
Tanzania.
“Lengo
letu ni kuisaidia Tanzania kwa kuuleta nchini uwekezaji unaohitajika
sana na kupunguza gharama za kukopa. Sisi ni watu wakimya lakini ni
sehemu muhimu sana ya fumbo kwa sababu tumesimama nyuma ya uwekezaji na
biashara ambayo inakadiriwa kufikia dola bilioni (2tr/-) nchini Tanzania
tangu kuanza kwa biashara mwaka 2004”, alibainisha Ofisa Mtendaji Mkuu
wa ATI George Otieno.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) George
Otieno akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano
maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza
wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa
la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji
kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na
ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es salaam.
Tusekile Kibonde ambaye ni Underwriter Responsible for Tanzania Kutoka
ATI akieleza maswala mbalimbali mbele ya wanahabari juu ya Mkutano huo
ambao unafanyika Jijini Dar es salaam ambapo Jukwaa hilo linawakutanisha
pamoja wadau kutoka Nyanja binafasi za umma katika kutafuta masuluhisho
ambayo yataondoa hatari zinazoikabili sekta ya nishati ili kuvutia
uwekezaji unaohitajika sana.
Kamishna msaidizi wa Umeme wa wizara, mhandisi Innocent Luoga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. Tanzania inaweza kunufaika zaidi kutokana na ubia wake na ATI kirahisi kwa kurudia utekelezaji wa ahadi zake kwa kusaidia miradi inayoungwa mkono na ATI ndani ya Tanzania. Chini ya masharti ya ubia, Tanzania inaweza kuwepo kiwango mbadala wa vipimo vya viwango kwa kipimo cha uwekezaji cha ATI daraja A mara tutakaposaini manunuzi yanayoungwa mkono na ATI.

Chini
ya kanuni za Basel, ambazo zinasimamia mabenki mengi ya kimataifa,
ynaweza kuikopesha nchi kama Tanzania ikiwa inaungwa mkono katika bima
na taasisi kama ATI, ambayo ni taasisi inayoheshimika na inayoaminiwa na
masoko ya kimataifa ya fedha. Bima ya ATI inaiwezesha benki kupunguza
kiwango cha mwisho cha malipo ya bima, ambacho kwa kiwango kikubwa
kinapunguza gharama za kukopa kwa Tanznaia na nchi nyingine za Afrika
ambazo ni wanachama.
Kushindwa
kutumia kikamilifu fursa hii, Tanzania inaweza kukosa uwekeza wenye
thamani ya mamilioni ya fedha. “ATI inaweza kuisaidia nchi kuwa inavutia
kuwekeza kifedha kwa kuvutia uwekezaji zaidi. Hili ni muhimu hususani
katika sekta ya nishati ambayo kwa hivi sasa ina ushindani mkubwa,”
alisema Mdhamini Mkazi wa ATI nchini Tanzania Tusekile Kibonde.
No comments:
Post a Comment