NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI NCHI AONGOZA WATUMISHI WA WIZARA YAKE KUAGA MWILI WA MWANASHERIA, MAREHEMU YUSTA MSOKA, JIJINI DAR
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akiaga mwili wa Mwanasheria wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma ya Mapfa, ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara hiyo, Jane Massawe.
Mkurugenzi wa Idara
ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba, Afisa Sheria
wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa wakiaga mwili wa mwanasheria mwenzao
wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita
na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Idara
ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba, akikabidhi
rambirambi kwa niaba ya Ofisi ya Mwajiri wa Afisa Sheria, marehemu Yusta
Msoka. Kushoto anayepokea rambirambi hiyo ni Mama wa marehemu huyo.
Mtumishi huyo alifariki dunia wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es
Salaam jana.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), tawi la Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi akisoma wasifu wa Afisa Sheria wa
Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita
na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (kushoto kwa
Balozi), Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba
wakiwa katika hali ya huzuni pamoja na waombolezaji wengine wakati wa
kuaga mwili wa marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita
na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment