DC MTATURU AWAONYA WANASIASA WANAOWAZUIA WANANCHI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka
akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Vitongoji, Kata na Vijiji katika
ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jinsi
ujenzi wa maabara unavyosuasua katika shule ya sekondari Mkunguakihendo
ambapo amemuagiza Diwani kusimamia ujenzi huo uli kufikia mwakani
maabara ianze kutumika
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua
utengenezaji wa Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo Kijiji cha
Itagata, Kata ya Kikio
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, akiwakwenye picha
ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,
Wakuu wa Idara na Vitengo, Diwani wa kata ya Kikio Steven Sinda, Walimu
na Viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata ya Mkunguakihendo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa shule ya Awali na Msingi Simbikwa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Misughaa Kata ya Misughaa
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo walimu walioalikwa kwenye kikao
cha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kilichofanyika
katika ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitafsiri kwa
vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi iliyoshinda uchaguzi uliofanyika
Octoba 25, 2015
Baadhi ya wakazi wa kijiji Cha Misughaa Kata ya Misoghaa wakimsikiliza
kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo
Dc Mtaturu akizungumza na wajasiriamali wanazalisha Chumvi katika Mbuga
ya Mwakilongo iliyopo katika Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio ambapo
amemtaka Afisa Ustawi wa jamii kuhakikisha vikundi vinasajiliwa kwa
ajili ya kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi na wenye tija
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa
maabara katika Shule ya Sekondari Dkt Shein iliyopo Kata ya Misughaa
ambapo pamoja na kupatikana jumla ya shilingi milioni saba kwa ajili ya
ujenzi wa maabara hiyo lakini bado hata msingi haujakamila, hivyo agizo
limetolewa kwa kufanyika uchunguzi wa namna zilivyotumika fedha hizo
Wananchi wa Kijiji cha Misughaa wakisikiliza kwa makini maagizo ya
serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
wakati wa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo
Na Mathias Canal, Singida
Wananchi wametakiwa kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kwa kuwataka kutochangia shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia ujenzi wa maabara kwani kufanya hivyo ni kuwapumbaza wananchi ilihali wanasiasa hao wanaofanya hivyo wamesoma na kufikia kuwa na nafasi nzuri kwenye serikali ambapo pia watoto wao wana elimu nzuri na wengine wanasoma nje ya nchi.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika ziara yake ya kikazi iliyoanza leo katika Kata mbili za Kikio na Kata ya Misughaa.
Dc Mtaturu amewataka viongozi hao kutoyakimbia maeneo yao ya kazi ikiwemo majimbo na kuachana na uongozi wa sifa zisizokuwa na tija badala yake wanapaswa kurejea Katika maeneo yao ya utendaji ili kushiriki kwa pamoja na wananchi katika shughuli za Maendeleo.
Mraturu ambaye ameanza ziara hiyo ikiwa na engo la kutembelea miradi ya maendeleo na kujua maeneo yote anayofanyia kazi, Kuhimiza shughuli za Maendeleo na kuwakumbusha wanasiasa kuwa uchaguzi mkuu ulifanyika Octoba 25 Mwaka jana na kumalizika hivyo wakati huu ni wa kufanya kazi na kuzikabili changamoto zinazowatatiza watanzania kwa miaka mingi.
Amesema kuwa serikali inaposema wananchi wachangie shughuli za maendeleo haina maana kwamba wananchi wachangie pesa pekee bali wanaweza kuchangia mchanga, Tofali na nguvu zao katika kuhakikisha Vitongoji na Vijiji vyao vina imarika katika miradi mbalimbali yenye tija katika jamii.
Dc Mtaturu amewataka wanasiasa kutojificha kwenye kichaka cha Demokrasia huku hawana nidhamu badala yake kuihubiri demokrasia kwa kufanya shughuli za kuwawezesha wananchi kuimarika katika shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri nchini Tanzania.
Ameahidi kuwavalia njuga baadhi ya wataalamu wote walioajiriwa na serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lakini wamebadili muelekeo na kuanza kufanya shughuli za siasa badala ya kuzitendea haki taaluma zao katika kuyafikia matokeo makubwa ya kipato cha wananchi.
"Watumishi wote wa serikali, Wakuu wa idara na vitengo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wanapaswa kufanya kazi moja tu ya kutafsiri kwa vitendo ilani iliyoshika hatamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Alisema Mtaturu
Sambamba na hayo pia amewasihi wananchi kutokata miti ovyo kwani jambo hilo litapelekea kukosekana kwa mvua za kutosha na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi badala yake wanapaswa kupanda miti zaidi katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya mashamba.
Dc Mtaturu ameahidi kushirikiana na viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuchochea shughuli za maendeleo na sio kushughulika na viongozi wa vyama kwani muda wa kuhangaika na vyama ni wakati wa kampeni zingine kwa ajili ya uchaguzi.
Dc Mtaturu kabla ya kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara ametembelea na kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Mkunguakihendo na Shule ya Sekondari Misughaa.
Amesema kuwa ni jambo la aibu kwa baadhi ya wanasiasa ambao wamegeuka kuwa matapeli wa hoja kwa kuwahadaa wananchi na kupotea katika maeneo yao ya kazi lakini huibuka tena wakati wa kampeni.
Kwa upande wa wananchi waliopata wasaa wa kuuliza maswali wamemtaka mkuu huyo wa Wilaya kuwasaidia katika kuimarisha uchumi na shughuli za maendeleo ya wananchi kwani Wilaya ya Ikungi imedumaa kimtazamo wa maendeleo tangu mwaka 2011 mpaka sasa.
Katika sekta ya Kilimo Dc Mtaturu ameitaja Pamba inayozalishwa Wilayani Ikungi kuwa ni ya kiwango cha ubora wa hali ya juu (Grade One) kitaifa hivyo amewataka wananchi hao kuongeza zaidi uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa kupitia zao hilo la biashara.
Dc Mtaturu amesema kuwa kwa mujibu wa kampuni inayosimamia kilimo hicho ya BioSuston imeeleza kuwa msimu uliopita ulikuwa na mafanikio makubwa kwa wakulima wa pamba Wilayani Ikungi ambapo hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi kumpeleka Afisa Kilimo awasaidie zaidi kuwapa mbinu bora za kilimo ili kuimarisha kilimo hicho na kupata mazao mengi yenye tija.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameagiza kuhamishwa kituo cha kazi mganga Mkuu wa Zahanati ya Misughaa Steven Kirita aliyafanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 katika kituo hicho huku akihusishwa na tuhuma za ulevi uliokithiri.
KAWAIDA..! DC MTATURU AWAONYA WANASIASA WANAOWAZUIA WANANCHI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Vitongoji, Kata na Vijiji katika ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi Wananchi wakisikiliza kwa makini maagizo ya serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jinsi ujenzi wa maabara unavyosuasua katika shule ya sekondari Mkunguakihendo ambapo amemuagiza Diwani kusimamia ujenzi huo uli kufikia mwakani maabara ianze kutumika Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua utengenezaji wa Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, akiwakwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Diwani wa kata ya Kikio Steven Sinda, Walimu na Viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata ya Mkunguakihendo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa shule ya Awali na Msingi Simbikwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Misughaa Kata ya Misughaa Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo walimu walioalikwa kwenye kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitafsiri kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi iliyoshinda uchaguzi uliofanyika Octoba 25, 2015 Baadhi ya wakazi wa kijiji Cha Misughaa Kata ya Misoghaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Dc Mtaturu akizungumza na wajasiriamali wanazalisha Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo katika Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio ambapo amemtaka Afisa Ustawi wa jamii kuhakikisha vikundi vinasajiliwa kwa ajili ya kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi na wenye tija Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Dkt Shein iliyopo Kata ya Misughaa ambapo pamoja na kupatikana jumla ya shilingi milioni saba kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo lakini bado hata msingi haujakamila, hivyo agizo limetolewa kwa kufanyika uchunguzi wa namna zilivyotumika fedha hizo Wananchi wa Kijiji cha Misughaa wakisikiliza kwa makini maagizo ya serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo Na Mathias Canal, Singida Wananchi wametakiwa kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kwa kuwataka kutochangia shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia ujenzi wa maabara kwani kufanya hivyo ni kuwapumbaza wananchi ilihali wanasiasa hao wanaofanya hivyo wamesoma na kufikia kuwa na nafasi nzuri kwenye serikali ambapo pia watoto wao wana elimu nzuri na wengine wanasoma nje ya nchi. Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika ziara yake ya kikazi iliyoanza leo katika Kata mbili za Kikio na Kata ya Misughaa. Dc Mtaturu amewataka viongozi hao kutoyakimbia maeneo yao ya kazi ikiwemo majimbo na kuachana na uongozi wa sifa zisizokuwa na tija badala yake wanapaswa kurejea Katika maeneo yao ya utendaji ili kushiriki kwa pamoja na wananchi katika shughuli za Maendeleo. Mraturu ambaye ameanza ziara hiyo ikiwa na engo la kutembelea miradi ya maendeleo na kujua maeneo yote anayofanyia kazi, Kuhimiza shughuli za Maendeleo na kuwakumbusha wanasiasa kuwa uchaguzi mkuu ulifanyika Octoba 25 Mwaka jana na kumalizika hivyo wakati huu ni wa kufanya kazi na kuzikabili changamoto zinazowatatiza watanzania kwa miaka mingi. Amesema kuwa serikali inaposema wananchi wachangie shughuli za maendeleo haina maana kwamba wananchi wachangie pesa pekee bali wanaweza kuchangia mchanga, Tofali na nguvu zao katika kuhakikisha Vitongoji na Vijiji vyao vina imarika katika miradi mbalimbali yenye tija katika jamii. Dc Mtaturu amewataka wanasiasa kutojificha kwenye kichaka cha Demokrasia huku hawana nidhamu badala yake kuihubiri demokrasia kwa kufanya shughuli za kuwawezesha wananchi kuimarika katika shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri nchini Tanzania. Ameahidi kuwavalia njuga baadhi ya wataalamu wote walioajiriwa na serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lakini wamebadili muelekeo na kuanza kufanya shughuli za siasa badala ya kuzitendea haki taaluma zao katika kuyafikia matokeo makubwa ya kipato cha wananchi. "Watumishi wote wa serikali, Wakuu wa idara na vitengo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wanapaswa kufanya kazi moja tu ya kutafsiri kwa vitendo ilani iliyoshika hatamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Alisema Mtaturu Sambamba na hayo pia amewasihi wananchi kutokata miti ovyo kwani jambo hilo litapelekea kukosekana kwa mvua za kutosha na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi badala yake wanapaswa kupanda miti zaidi katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya mashamba. Dc Mtaturu ameahidi kushirikiana na viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuchochea shughuli za maendeleo na sio kushughulika na viongozi wa vyama kwani muda wa kuhangaika na vyama ni wakati wa kampeni zingine kwa ajili ya uchaguzi. Dc Mtaturu kabla ya kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara ametembelea na kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Mkunguakihendo na Shule ya Sekondari Misughaa. Amesema kuwa ni jambo la aibu kwa baadhi ya wanasiasa ambao wamegeuka kuwa matapeli wa hoja kwa kuwahadaa wananchi na kupotea katika maeneo yao ya kazi lakini huibuka tena wakati wa kampeni. Kwa upande wa wananchi waliopata wasaa wa kuuliza maswali wamemtaka mkuu huyo wa Wilaya kuwasaidia katika kuimarisha uchumi na shughuli za maendeleo ya wananchi kwani Wilaya ya Ikungi imedumaa kimtazamo wa maendeleo tangu mwaka 2011 mpaka sasa. Katika sekta ya Kilimo Dc Mtaturu ameitaja Pamba inayozalishwa Wilayani Ikungi kuwa ni ya kiwango cha ubora wa hali ya juu (Grade One) kitaifa hivyo amewataka wananchi hao kuongeza zaidi uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa kupitia zao hilo la biashara. Dc Mtaturu amesema kuwa kwa mujibu wa kampuni inayosimamia kilimo hicho ya BioSuston imeeleza kuwa msimu uliopita ulikuwa na mafanikio makubwa kwa wakulima wa pamba Wilayani Ikungi ambapo hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi kumpeleka Afisa Kilimo awasaidie zaidi kuwapa mbinu bora za kilimo ili kuimarisha kilimo hicho na kupata mazao mengi yenye tija. Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameagiza kuhamishwa kituo cha kazi mganga Mkuu wa Zahanati ya Misughaa Steven Kirita aliyafanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 katika kituo hicho huku akihusishwa na tuhuma za ulevi uliokithiri.

No comments:
Post a Comment