WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AUNGANA NA WAISLAMU KATIKA SWALA YA IDD EL HAJI VIWANJA VYA MWEMBE YANGA, TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (kushoto),
na Sheikh Ponda Issa Ponda, wakiomba dua wakati wa swala ya Idd El Haji
kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo
Septemba 12, 2016. (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka waumini
wa dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda mema na kuungana
na waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri
Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd el Haji
iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam
ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo ni pamoja na Sheikh
Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara), Sheikh Ponda Issa Ponda na
Sheikh Rajab Katimba.
“Kwa
niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu njema, na ninaomba kuwasilisha salamu
za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph
Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, na niwaombe
ndugu zangu muitumie sikukuu hii kudumisha amani na upendo.” Alisema Waziri
Mkuu.
Waziri
M,uu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini,
kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi
lililosababisha vifo.
Waziri
Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja wa
michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11, 2016,
alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa matibabu.
Tetemeko hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi
alasiri Septemba 10, 2016.
Naye
mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa
kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika swala hiyo
ya Idd. “Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu kwa kutoka Oysterbay
hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika kutekeleza swala hii ya Idd El
Haji, mwenyezimungu amjalie heri na busara katika uongozi wake,” Alsiema Sheikh
Kishki.
Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
Muumini wa Kiislamu akiomba dua
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mikono na Sheikh Ponda Issa Ponda, mara baada ya swala hiyo
Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda
Waziri Mku, akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Shariff, (kushoto), na Sheikh Nurdin Kishki
Waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye swala
Waumini wa Kiislamu, wakiomba dua
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
(katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Masheikh na viongozi wa
serikali mara baada ya swala hiyo
Sheikh Nurdin Kishki, akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa swala ya Idd El Haji
viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam
Sheikh Nurdin Kishki, kiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, wakati wa swala hiyo
Watoto hawa wa Kiislamu, wakionyesha
furaha baada ya kushiriki swala ya Idd El Haji, (Mlulu Khalfan (kushoto)
na mdogo wake Kuugara.
No comments:
Post a Comment