Viongozi wapya wa KIDIFA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege
Mwenyekiti wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi
Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
MTANGAZAJI
nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA)
katika uchaguzi uliofanyika jana.
Jesse ambaye aliupata
uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka
kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge
aliyepata kura 21.
Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo
alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis
Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi
Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
Wasimamizi
wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA),
Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina
Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
Mwakilishi wa
klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka
Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu
alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa
alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
Mwenyekiti wa KIDIFA
aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe
aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika
soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo
la kutafuta vipaji.
Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi
kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu
ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine
zinashiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti Jesse alisema
wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini
vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia
miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.
No comments:
Post a Comment