GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULU ASEMA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA NI IMARA, ASEMA "WAPIGA DILI" WAMEDHIBITIWA
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Museum wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016 kuhusu hali ya uchumi wa taifa. (PICHA NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
GAVANA
wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, amesema hali ya uchumi wa
Tanzania ni ya kuridhisha tofauti na taarifa zinazozagaa kuwa uchumi wa nchi umedorora.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Museum
wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Septemba 14, 2016, Gavana huyo alisema,
hali ya uchumi ni imara kwa vile tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano,
mfumuko wa bei umedhibitiwa na unashuka siku hadi siku hali kadhalika, thamani
ya shilingi nayo inaendelea kuimarika.
Profesa
Ndulu pia alisema,si kweli kwamba, fedha zimepungua mitaani bali fedha zipo ila
fedha za “dili”ni kweli “zimekauka” na hii ni kutokana na jitihada za serikali
katika kuziba mianya ya rushwa, wakwepa kodi na matumizi mabaya fedha za umma.
Aliwatoa
hofu wananchi kwa kusema kuwa, hali ya uchumi wetu itaendelea kuimarika katika mwaka
2016 kutokana na viashiria kadhaa ambavyo ni pamoja na uzalishaji wa umeme
katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, umeongezeka kwa asilimia 14.5 kufikia KwH milioni
3,454.2 ikilinganishwa na na kWh milioni
3,016.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Akifafanua
zaidi alisema, ongezeko hilo la umeme limetokana na jitihada za serikali katika
kutumia nishati ya gesi kwenye uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba
la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi
I. “Umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia
52.2, hali itakayosaidia kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na sekta
nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na hivyo kuchangia katika kuongeza
pato la Taifa na pia ghjarama ya umeme itashuka.” Alisema.
“Kumekuwepo
na taarifa nyingi zinazozagaa kuwa uchumi umedorora, lakinikwanza napenda
niweke wazi, mimi si mwanasiasa, mimi nataka kulizungumzia swala hili
kitaalamu, ukiangaliatakwimu za Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuajiwa
uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha, katika robo ya kwanza ya
mwaka 2016, ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko
la asilimia 5.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015, sasa kwa takwimu hizi
hauwezi kusema uchumi umedorora, hii si kwelikabisa,” alisema Profesa Ndulu.
Taarifa
kamiliya Profesa Benno Ndulu kuhusu hali ya uchumi soma hapo chini.
Profesa Ndulu na wasaidizi wake kutoka
kushoto, Meneja Uhusiano na masuala ya peotokali, Zaria K. Mbeo,
Mkurugenzi wa Sera na Uchumi, Johnson Nyela, Mkurugenzi wa Usimamizi wa
Mabenki, Kened A. Nyoni, wakinakili maswali toka kwa waandishi wa habari
Profesa Ndulu akizungumza |
Bibi Mbeo |
Taarifa ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu kwa Waandishi wa habari hii hapa ch
No comments:
Post a Comment