WATANZANIA TUPAZE SAUTI KUKATAA MAANDAMANO YA SEPTEMBA MOSI-CHEYO
Mwenyekiti
wa UDP Mh. John Cheyo akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo
pichani)kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini
Dar,akiwaomba viongozi wa chama cha CHADEMA,Kusitisha maandamano yao
waliyoyapa jina la UKUTA,wanayotarajia kuyafanya Septemba Mosi nchi
nzima,Mh Cheyo amekiomba chama hicho kutofanya maandamano hayo kwa
lazima na badala yake watumie njia ilio sahihi ambayo ni ya mazungumzo
ya mezani na kuendelea kuitunza amani ya nchi iliopo,pia amewaomba
Watanzania kupaza sauti zao kuyakataa maandamano hayo yanayoweza
kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu.Pichani kulia ni Kaimu Katibu
MKuu wa chama hicho Mh,Goodluck Ole Medeye.
"Ukitaka
kufanya maandamano,vyombo vya usalama vikikukatalia,basi usitumie
nguvu,jaribu kutafauta njia nyingine ambayo itakuwa ya amani zaidi
kuliko kulazimisha,jambo ukililazimisha bila kufuata taratibu na sheria
za nchi,matokeo yake hayatakuwa mazuri,yataleta machafuko na kutia doa
amani ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijivunia,hivyo nawasihii ndugu
zangu wa CHADEMA bado kuna njia nzuri za kufuata na kufikia muafaka wa
jambo hilo bila kusumbua amani ya nchi yetu iliopo kwa sasa" alisema Mh
Cheyo.
Mh,Cheyo
akisitiza jambo wakati alipokuwa akijiabu maswali mbalimbali ya
waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kukitaka chama cha
CHADEMA kusitisha maandamano yake,kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Habari MAELEZO,Vicent Tinganya.PICHA NA MICHUZI JR.
Na: Lilian Lundo-MAELEZO
Dar Es Salaam
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na
kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na
Chama cha Demokrasia (CHADEMA).
Cheyo
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.
“Watanzania
wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si
jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya
Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.
Alisema
kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua
migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo
yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.
Aliongeza
kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii
uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama
hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri
anayehusika na Jeshi la Polisi.
Akifafanua
zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za
kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo
viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na
kujihusisha na masuala ya rushwa.
Mwenyekiti
huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili
aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya
Tanzania.
Aidha
Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi
lolote. Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la
amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
No comments:
Post a Comment