MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA LINDI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Kagwa.
Mkuu
wa mkoa wa Lindi Ndugu Godfrey Zambi akisoma taarifa ya mkoa wakati wa
mkutano uliowakutanisha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la
Mtakatifu Andrea Kagwa.
Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi waliohudhuria mkutano wao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
---
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza
viongozi wa mkoa wa Lindi wasimamie kikamilifu zoezi la utengenezaji wa
madawati ili kuhakikisha madawati yanayotengenezwa yanakuwa na ubora na
yanakidhi viwango vinavyotakiwa
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Lindi Tarehe 7-Aug-2016
katika mkutano wake na wajasiriamali wa mkoa Lindi pamoja na viongozi
mbalimbali wa mkoa huo.
Makamu wa
Rais amesema msukumo mkubwa wa serikali uliopo kwa sasa unalenga kuhakikisha
madawati yanayotengenezwa kote nchini yanakuwa imara huku akipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya
mkoa wa Lindi ya utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa mkoa huo umebakisha
asilimia Moja tu ya utengenezaji wa madawati hayo ili kukamilisha zoezi hilo.
Kuhusu mikopo
kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali
italifanyia kazi ombi la wajasiriamali wa mkoa wa Lindi ambao wameiomba
serikali ifanye mazungumzo na watendaji wa taasisi za kifedha nchini ili waweze
kupunguza riba kwenye mikopo wanayopata kama hatua ya kuongeza hamasa kwa
wananchi wengi zaidi kukopa fedha kwa ajili ya kuimarisha shughuli ujasiriamali.
Makamu wa
Rais pia amezitaka halmashauri zote nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kutenga
asilimia TANO ya makusanyo ya mapato yake na kutoa fedha hiyo kwa wanawake na
vijana kwenye halmashauri hizo ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi yao ya
kiuchumi kwenye maeneo yao.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment